Sunday, March 8, 2015

Unamjua padri feki?

SIRI ya mafanikio ya Padri feki, Josephat Asenga, aliyekamatwa mkoani Morogoro, katika kuongoza Misa ya Kanisa Katoliki kwa kufuata taratibu zote maalumu bila kutiliwa shaka, imebainika. Asenga aliyetumia vitambulisho feki, alipojitambulisha kwa uongozi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Maria Madeko mkoani Morogoro, alipopewa fursa ya kuongoza Misa, alitekeleza wajibu huo wa kipadri bila kuacha shaka. *Alivyojitambulisha Akizungumza na gazeti hili jana, kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki (jina limehifadhiwa), alithibitisha kuwa Asenga alipofika Parokiani hapo kati ya Mei na Juni mwaka jana, hakutiliwa shaka hata kidogo kuwa si Padri. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Asenga alifika kanisani hapo akiwa amevaa mavazi ya kipadri na kujitambulisha kuwa yupo nchini kwa mapumziko, akitokea nchini Marekani, alikodai ndipo anakofanyia shughuli zake za upadri katika Jimbo Kuu la New York. Mbali na kuvalia mavazi ya kipadri, Asenga pia alionesha kitambulisho na kusababisha uongozi uamini kuwa ni Padri na kumpa makaribisho ya Padri mwenzao. “Alipoonesha kitambulisho tulimwamini na jinsi alivyokuja na mavazi ya upadri na muonekano wake alionao, haikuwa rahisi kumtilia shaka,” alisema kiongozi huyo. *Kuongoza Misa Baada ya kupata makaribisho ya kipadri, Asenga kwa mujibu wa kiongozi huyo, aliomba apangiwe zamu ya kuongoza misa ya Jumapili iliyofuata na kukubaliwa. Kiongozi huyo alithibitisha kuwa Asenga aliongoza vyema misa hiyo, kwa kufuata taratibu zote za kanisa hilo kama zinavyofuatwa na mapadri wengine. Taratibu Kwa kawaida Misa katika Kanisa la Katoliki, huanzia Sakestia, sehemu ambayo mapadri na waministranti, ambao ni wasaidizi wao, huvaa majoho na kusali kabla ya kuingia kanisani wakisindikizwa na nyimbo. Baada ya kuingia madhabahuni, Padri hubusu madhabahu kabla ya kualika waumini katika Misa. Mualiko huo hufuatiwa na maelezo kidogo na kuanza Ibada ya Kitubio, ambayo waumini hutubu dhambi zao na kujiweka tayari kusikiliza neno la Mungu. Ibada ya kusomwa neno, kwa kawaida masomo matatu kutoka vitabu vya Agano la Kale na Jipya katika kitabu cha Bibilia Takatifu, Padri huanza kutoa mahubiri. Mahubiri yakiisha, Misa huendelea kwa sadaka na baadaye, Padri huongoza waumini kuanza kukumbuka maelezo ya siku ambayo Yesu Kristo alitoa Sakramenti katika Chakula cha Mwisho kwa wanafunzi wake akitaka wamkumbuke. Kwa kawaida, eneo hilo ndipo Padri kwa mamlaka aliyopewa, hufanya mageuzi ya sakramenti kuwa Hostia Takatifu, kwa maneno mengine hubariki mkate kuwa Mwili wa Kristo na divai kuwa Damu ya Kristo. Kwa Wakatoliki, eneo la mageuzi ni eneo muhimu na ndio waumini hutuma maombi kimya kimya, wakiamini ndio Kristo anashuka mwenyewe. Baada ya kutumikia Kanisa na kukubalika, Asenga aliaga kuwa anarudi nchini Marekani kwa kuwa muda wake wa mapumziko, umekwisha na kuagwa na Kanisa. Taarifa tata Wakati uongozi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Maria Madeko, ukiwa na imani kuwa Asenga ni Padri na amerejea New York, kuendelea na Utume, walipata taarifa za kushangaza kutoka kwa baadhi ya waumini, wakidai wamekutana na Asenga mitaani. Mbali na taarifa hiyo ya kukutwa mitaani na waumini wake, taarifa zaidi zilieleza kuwa amekuwa akiishi na mwanamke katika eneo la Ujenzi, kinyume na desturi za mapadri wa Kanisa Katoliki duniani, ambao hawaruhusiwi kuoa. *Mtego 1 Baada ya taarifa hizo, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, Asenga aliwekewa mtego na Paroko wa Parokia hiyo ya Mtakatifu Maria Madeko, Malt Dyfrig Joseph. Paroko huyo inadaiwa aliwaomba waumini wamshawishi Asenga afike parokiani hapo na baada ya kufika, alihojiwa na Paroko huyo na kudai kuwa alipata upadirisho katika Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya Paroko huyo kupata maelezo hayo, alifanya mawasiliano na Katibu wa Jimbo hilo la Dar es Salaam na kujibiwa kuwa hakuna jina la Padri huyo. Kukamatwa, akiri Mtego wa pili kwa mujibu wa Kamanda Paulo, ulifuata kwa Paroko huyo kutoa taarifa Polisi kuhusu uwepo wa Padri feki, ambaye aliaminiwa kwa kiwango cha kuruhusiwa kuongoza Misa. Taarifa hizo zinasema Alhamisi ya wiki hii, saa 10:30 jioni, Asenga alimpigia simu Paroko huyo na kuomba ampangie kazi ya kuendesha Misa Jumapili ya leo parokiani hapo, na kukubaliwa ambapo Paroko huyo alimtaka afike kanisani. Baada ya kufika, taratibu za kujulisha Polisi zilifanywa na askari walipofika kanisani hapo, walimkamata mtuhumiwa huyo. Kwa mujibu wa Kamanda Paulo, baada ya kufanya mahojiano na Asenga, alikiri kuwa yeye si Padri na walipokwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi, walimkuta akiwa na majoho saba ya upadri. Mikoani, mafunzo Taarifa zaidi zilizofikia gazeti hili jana, zilibainisha kuwa Asenga huenda kwa kutumia mbinu hizo hizo, alishaaminiwa kuongoza Misa katika mkoa wa Kilimanjaro katika maeneo ya Uru na Moshi na mkoani Singida. Mbali na kukubalika katika mikoa hiyo, lakini taarifa zaidi zilibainisha kuwa Asenga alifanikiwa kote huko kuongoza Misa na kuaminiwa, kutokana na mafunzo ambayo aliwahi kupata huko nyuma. Inadaiwa Asenga alianza kupata mafunzo katika Seminari ya Kanisa Katoliki ya Uru, ambako alipata mafunzo ya elimu ya sekondari. Baada ya kumaliza kwa mafanikio masomo yake katika seminari hiyo, alichaguliwa kujiunga na Seminari ya Kibosho, ambayo inatajwa kuwa maalumu kwa ajili ya kutoa elimu ya falsafa kwa wanafunzi na wengi ni wanaotarajiwa kuwa mapadri. Mafanikio aliyoyapata katika masomo ya falsafa katika Seminari ya Kibosho, yalimwezesha kujiunga na Seminari ya Kipalapala, ambako inaelezwa ndiko kunakotolewa mafunzo ya Liturgia, ambayo nayo ni sehemu ya mafunzo wapewayo wanafunzi wanaotarajiwa kuwa mapadri. Waumini Ingawa taarifa za mafunzo aliyopata zinatiliwa shaka, lakini namna alivyoongoza Misa bila kutiliwa shaka, imesababisha baadhi ya waumini kuanza kumjadili, ili kufahamu hasa nia yake ilikuwa ipi. Kutokana na taaluma nyingine aliyonayo ya uhasibu, amesababisha baadhi ya waumini kuunganisha matukio na uwezo wake na kuamini kuwa huenda hakuwa akitafuta sadaka. Mmoja wa waumini aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alidai kuwa huenda Asenga alikuwa na njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Kwa mujibu wa madai ya muumini huyo, watu wa aina ya Asenga, ambaye ana taaluma na uwezo wa kipadri, wana njia nyingi za kujipatia kipato, hivyo inawezekana alidanganya wafadhili wake kuwa yeye ni Padri ili apate ufadhili huo. Muumini huyo alikwenda mbali na kudai huenda masharti ya ufadhili huo, ni kupata picha au sauti yake akiongoza Misa kanisani. “Inawezekana kuna mahali aliomba ufadhili kwa ajili ya kitu fulani na aliwadanganya kuwa yeye ni Padri, ndio maana akaamua kuomba zamu ya kuongoza Misa. “Utapeli umeingia mpaka kwenye nyumba za ibada kweli? Wanadamu tumekosa hofu ya Mungu!” Alihoji muumini huyo na kuasa jamii kuwa macho, kwa kuwa hivi sasa matapeli ni wengi na kila siku wanatoka na mbinu mpya. Credit:Habari Leo

Milipuko yawaua watu 50 Nigeria

Zaidi ya watu 50 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya mabomu yaliyofuatana siku ya jumamosi kwenye mji wa maiduguri ambo ndio chimbuko la Boko Haram. Milipuko mitano ilitokea ndani ya saa moja kwenye masoko yenye shughuli nyingi pamoja na kwenye kituo cha basi. Serikali ya Nigeria inasema kuwa boko haram wanaendesha mashambulizi hayo kwa sababu inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa jeshi. Jeshi la Nigeria likisaidiwa na la Chad , Cameroon na Niger limejaribu kupambana na wanamgambo wa boko haram kuwaondoa kutoka ngome zao kabla ya uchaguzi ambao utafanyika baadaye mwezi huu.

HATIMAYE MOTO UMEZIMWA JIJINI CAPE TOWN

Moto mkubwa ambao uliwaka usiku wa kuamkia jumatatu umezimwa.. moto huo ambao uliwaka kwa muda wa siku6 mfululizo umeteketeza eneo kubwa la msitu uliopo katika milima ya muizinberg na southern peninsula.. eneo hilo la milima lina aina mbali mbali ya viumbe kama vile sokwe,mbwa mwitu,myani na kobe.. mpaka sasa bado halmashauri y jiji la cape town halijasema ni hasara ya kiasi gani imeopatikana kutokana na moto huo.

''JIHAD JOHN'' Chinja chinja wa IS alifukuzwa Tanzania

Mohammed Emwazi ,mtu ambaye alibadilika na kuwa ''chinja chinja'' wa kundi la islamic state kwa jina 'jihad John' Mohammed Emwazi, alifurushwa kutoka nchini Tanzania kwa kuwa mlevi na mtu anayetoa matusi.,afisa moja wa polisi ameiambia BBC. Emwazi anasema alitishiwa na kuhojiwa chini ya maagizo ya shirika la upelelezi la Uingereza MI5 alipoenda nchini humo mwaka 2009 Lakini BBC imeonyeshwa rekodi za kuzuiliwa kwake tangu alipokamatwa. Afisa huyo amesema kuwa Emwazi hakuruhusiwa kuingia nchini Tanzania kwa sababu alikuwa amezua mgogoro katika uwanja wa ndege na kuwa na tabia za mlevi. Emwazi ambaye ana zaidi ya miaka 20 na ambaye anatoka magharibi mwa London ametambuliwa kama mtu aliyeziba uso katika kanda kadhaa za video ambapo mateka wamechinjwa. Emwazi amesema kuwa alikuwa mwanafunzi ambaye alikuwa katika likizo ya safari wakati aliposafiri na kuingia Afrika mashariki kupitia uwanja wa ndege wa Dar-e-salaam kutoka nchini Uholanzi miaka sita iliopita.

Wednesday, March 4, 2015

Kutana na Bilione Kijana Zaidi Afrika

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika. Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania . “Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,” inaongeza ripoti hiyo. Metl ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka. Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote. Kwa mujibu wa tovuti yake, Metl inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli. Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Dewji anashika nafasi mbili juu zaidi ya kada maarufu wa CCM na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Aziz Rostam (50) aliyewekwa nafasi ya mwisho. Rostam amefungana nafasi ya 26 na mabilionea wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu na Femi Otedola wenye utajiri wa Sh1.8 trilioni kila mmoja. Orodha hiyo ya 29 bora inaoongozwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote akiwa na utajiri wa Dola 15.7 bilioni za Marekani (Sh28.2 trilioni), kiwango ambacho ni mara moja na nusu ya bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka 2014/15. Forbes linamtaja Rostam kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.8 trilioni), kiwango ambacho kimebaki pasi na mabadiliko kutoka orodha ya mwaka jana. Rostam anamiliki asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Vodacom.

Monday, March 2, 2015

MOTO MKUBWA CAPE TOWN

Moto mkubwa ulioanza usiku wa kuamkia jumatatu umeenselea kuteketeza sehemu kubwa ya milima ya muizinberg mjini cape tow.. kwa mujibu wa mashuhuda wamedai kuwa imekuwa vigumu kuuzima moto huo kutokana na upepo mkali unaovuma eneo hilo.. mpaka majira ya sa8 mchana zaidi ya askari wa zimamoto 350 ,magari 60 na helikopta 6 zilikuwa katika shughuli nzito ya kuzima moto huo.. taarifa zinasema moto huo hautazimika kiurahisi kutokana na hali ya hewa na unaweza kuchukua siku 7 kuuzima moto huo..

Vikosi vya kuzima moto vyapata wakati mgumu kuzima moto Cape town

Zaidi ya helikopta 8 na magari 40 ya zimamoto na askari wa kikosi cha kuzima moto wapatao 200 wako katika jitihada za kuuzima Moto mkubwa unaowaka katika maeneo ya milima ya Muizinberg mjini Cape town,Moto huo ambao ulianza usiku wa jumapili umekuwa ukiwashinda nguvu kikosi hicho kutokana na upepo mkali unaovuma eneo hilo.! Mashuhuda wanasema kuwa watu wote wanaoishi maeneo yanayozunguka Eneo la moto wamehamishwa na kupelekwa eneo salama.! Mpaka sasa bado hakuna matumaini ya kuuzima moto huo ambapo helikopta za kuzima moto zimeonekana zikinyonya Maji katika Mabwawa ya kuogelea(swimming pools) katika maeneo hayo ili kurahisisha uzimaji wa moto huo..!

Sunday, March 1, 2015

Uchaguzi wa bunge waahirishwa Misri

Tume ya uchaguzi ya Misri inasema kuwa inatayarisha ratiba mpya ya uchaguzi wa wabunge ambao ukitarajiwa kufanywa badaae mwezi huu. Hapo awali mahakama kuu ya Misri yaliamua kuwa sehemu ya sheria kuhusu uchaguzi inakwenda kinyume na katiba na hivo kuzusha uwezekano wa kucheleweshwa. Rais Abdul Fattah al-Sisi alijibu hukumu hiyo kwa kuamrisha kuwa sheria mpya kuhusu uchaguzi itayarishwe katika mwezi mmoja. Bunge la Misri lilivunjwa mwaka wa 2012 baada ya kufutwa na mahakama. Na wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri imewasamehe na kuwaachilia huru wafungwa 68 kufuatana na msamaha aliotoa rais. Rais Abdul Fattah al-Sisi alitoa amri hiyo mwezi wa Januari kuadhimisha miaka mine baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani Rais Hosni Mubarak. Wafungwa wengine 72 wamefunguliwa kwa shuruti wasivunje sheria tena. Inafikiriwa kuwa wengi walioachiliwa huru walikuwa wafungwa wa kisiasa. Tangu Rais Sisi kushika madaraka waandamanaji kama 1,400 wameuliwa na askari wa usalama, na kama 40,000 wamekamatwa - wengi wao wanashutumiwa kuwa Waislamu

THE RETURN OF MWALIMU MKONJE ( THE BLOG )

Baada ya kimya cha muda mrefu sasa tunarudi hewani,kwa sasa tumefanikiwa kuwa na staf wanne ambao watahakikisha unapata habri kwa kadri zinavyowafikia