La hasha! Ni matunda ya kukua
kwa utandawazi. Mtanzania asiye
na pasport, leo anaweza akawa
na rafiki Australia ambaye
anakuwa anamjua kila
kinachoendelea katika Jiji la
Sydney. Hakuna gharama kubwa,
anajua yote kwa mtindo wa
kuchati kwenye ukurasa wa
Facebook.
Mtanzania akiwa nje ya nje,
akitaka kujua muhtasari wa kile
kinachoendela nchini kwake,
anaweza kutumia gharama
nafuu, kuulizia mazingira na
usalama wa taifa kupitia ukurasa
wa Facebook. Inapeleka watu
katika ulimwengu mpya,
inazidisha uhalali wa usemi
kwamba dunia ya sasa ni kama
kijiji kimoja.
Inasaidia kuongeza wigo wa
marafiki. Watu wanaweza
kubadilishana mawazo ya kijamii,
pia wakapeana uzoefu kwa
namna mbalimbali.
Inawakutanisha watu kwa njia
ya kipekee na kuwafanya
wazoeane kabla ya kugeuka
marafiki wakubwa.
INA ATHARI GANI KIMAPENZI?
Facebook imekuwa ikiwafanya
baadhi ya wanaume kuona njia
ya mkato kupata wapenzi wa
mbali. Akaunti yake inajaza
marafiki wa kike, hana mpango
na wanaume wenzake.
Wanakuza wigo wa kunufaika
katika ngono.
Msomaji na rafiki yangu, Shadya
Ismail aliniandikia ujumbe kwa
SMS ambao unasomeka hivi:
“Simu ni tatizo lakini huku
kwenye Facebook nako ni balaa.
Kusema ukweli, mimi nikigundua
mpenzi wangu anatumia muda
mwingi internet lazima
nimfuatilia nijue kinamsumbua
nini.”
Nilipomuuliza kwanini, alijibu:
“Hakuna amani Facebook.
Mwanaume anaomba urafiki kwa
mwanamke na anamkubalia.
Wakikutana online wanachati,
wanakubaliana baadhi ya vitu na
ikiwezekana wanapanga mpaka
miadi ya kukutana. Amini
kwamba hayo yapo na kuna
watu ni mfano.”
Nikamuomba ufafanuzi:
“Mapenzi ya siku hizi
hayatabiriki, nadhani ndiyo
maana tunaambiwa hizi ni
nyakati za mwisho. Watu
hawajuani lakini wanazoeana
kwa kuchati kisha wanakuwa
wapenzi. Nasema kwa kujiamini
kwa sababu nimetongozwa na
wengi.”
Anasimulia alivyotongozwa:
“Kuna wanaume watatu
waliniomba urafiki kwenye
Facebook. Mimi nikikuta ombi
nakubali. Siku tukikutana online,
tunachati vizuri lakini maswali
mengi yanakuwa yale binafsi
zaidi, yaani kama vile mtu
anataka kukujua sana.
“Nashindwa kutilia hofu,
kwahiyo najibu. Mwisho wa yote
anamalizia kwa kukutaka
kimapenzi. Watu watatu
wamenitongoza na kusitisha
urafiki nao. Ninao marafiki
wawili wa kike, mmoja amewahi
kulala kimapenzi na jamaa
aliyekutana naye Facebook,
alipopata penzi alianza mbele.
“Mwingine mpaka leo
anaendelea na mpenzi wake
ambaye walikutana Facebook.
Lakini huyo mpenzi wake ni
mume wa mtu, kwahiyo
wanaibana. Hapo utaona ni kwa
namna gani fursa za watu
kukaribiana kimapenzi
zimeongezeka hasa baada ya
Facebook kuchanua.”
SHADYA ANASEMA KWELI
Ni ukweli kwamba Facebook
inaumiza watu kwenye mapenzi.
Idadi ya watu wanaoanzisha
uhusiano mpya ni kubwa kila
siku kupitia kurasa hizo.
Uaminifu umekuwa ukipungua
na wasiwasi wa watu kwa
wapenzi wao ni kubwa.
Ninao mfano wa jamaa mmoja
ambaye kila anapofungua
ukurasa wa mwenzi wake, yeye
hukimbilia kuangalia marafiki
wapya ambao amewasajili.
Huumizwa mno anapogundua
kuna midume imo kwenye
orodha. Wanagombezana lakini
ushahidi wa kusaliti haupo.
Mwingine yeye hufuatilia namna
mwenzi wake anavyojadiliana na
marafiki zake katika mada
mbalimbali. Akiona picha ya
mpenzi wake imesifiwa mno na
mwanaume, anahoji:“Huyu
mbona amekusifia sana, ni nani
wako? Lazima mtakuwa
mnajuana, haiwezekani iwe hivi
hivi.”
SULUHISHO
Kila mmoja anatakiwa aishi kwa
maumivu ya mwenzi wake. Ni
vizuri pia akawa na uelewa
mpana kwamba hakuna kitu
kibaya kama kumfanya
mwenzako kuwa na wasiwasi na
wewe. Fanya kila uwezalo lakini
hakikisha mpenzi wako
anakuamini muda wote.
Atakuamini kama humpi sababu
ya kukutuhumu. Haoni tatizo
Facebook, rafiki mwenye
maneno yasiyofaa, jaribu
kumpotezea mapema.
Anapofungua ukurasa wako,
hakuti kitu kibaya zaidi ya
marafiki ambao mazungumzo ni
ya kawaida.
Kwanini ulegee kwa kuchati peke
yake? Onesha msimamo. Kama
wewe ni bachela si vibaya
ukianzisha uhusiano lakini ikiwa
una mwenzi wako, epuka.
Kumbuka kwamba jinsi ilivyo
kwako kupata mpenzi, naye
hivyo hivyo ni rahisi kunasa
wake. Unaona hatari iliyopo?
Uaminifu siyo tu kwamba ni kitu
muhimu, bali pia ni nguzo ya
uhusiano wowote ule. Ukiwa
chanzo wewe ukateleza,
utaachwa au ukisalitiwa
itakuuma na hata uamuzi
utakaouchukua, hautaweza
kufidia maumivu uliyoyapata.
No comments:
Post a Comment