Thursday, June 28, 2012
Ni ipi siri ya Muungano,Watanganyikawanaogopa nini ?
Leo ni takriban miaka 48 ya Muungano kati ya
Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Tanganyika tokea
kuasisiwa kwake baada ya Mapinduzi,lakini kwa
walio wengi hususani Wazanzibar wameshindwa
hasa kujua ni ipi hasa siri ya Muungano huu.Kumekuwa na madai mengi na fikra tofauti
kuhusu Muungano huu kutoka kwa watu na
taasisi mbali mbali ndani na nje ya nchi. Ni dhahiri
kwamba mwisho wa yote Muungano huu
utamalizika au utaendelea mbele ukiwa na
uhasama mkubwa kuliko udugu,upendo,maelewano na maendeleo kama
wanavyodai wale wote wenye hoja ambazo
wanautetea Muungano huu wenye hila na siri nzito,
hususani Viongozi wa Serikali walioko madarakani
wale wa Bara na baadhi ya wale Wahafidhina wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ambao hutumiwa kama chambo zidi ya Wazanzibar wenzao. Katika Muungano huu tokea siku ya mwanzo ,
kumekuwa na tuhuma nyingi kiasi ambacho kwa
mwenye akili timamu hatosita kuelewa kwamba
ndani yake kuna siri nzito zidi ya Taifa moja. Kwa
walio wengi wanakumbuka kwamba unapolitaja
neno Muungano hapo zamani ilikuwa ni kosa la jinai na adhabu yake kwa wakati huo ilikuwa
kifo.Wako Wazanzibar wengi ambao walikuwa
Wasomi,wanafalsafa,wanasiasa,madokta pamoja
na Wananchi wa kawaida walipoteza maisha yao
kwa kupinga au kuhoji Muungano huu,lakini kama
haya hayatoshi hadi hii leo bado Wazanzibar wanaonekana kama ni maadui pale tu
wanapoligusia suala zima la kudai haki yao ndani
ya Muungano. Tuangalie kama vile jumuia ya
Uamsho ambayo imejitolea kwa ridhaa yao
kuwaelimisha Wananchi juu ya haki zao za msingi
kudai Nchi yao huku wakifuata sheria za Nchi,hapa pana kuna kosa gani kwa Mwananchi kujielewa na
kujua haki zake za msingi? Nilifikiria ya kwamba
Serikali zote mbili zitawapongeza kwa vile Jumuiya
hiyo imejitolea kihali na mali kutoa elimu kwa
Wazanzibar, jambo ambalo Serikali zote mbili
zimeshindwa kulifanya kwa Wananchi wake. Kichekesho ni kuona Muungano huu wa Nchi mbili
huru, mara zote wanaolalamika kuonewa ni
upande mmoja wa Muunganoyaani Zanzibar, lakini
zaidi wanaopiga kelele kwa kuumia ni wananchi
wanyonge walio wengi na si Viongozi wa Serikali
zote mbili.Pia la ajabu ni kwamba Watanganyika wamerizika na wala Wananchi wake hawana madai
kwamba wanaonewa na zaidi wanapendelea
Muungano huu uzidi kuimarika. Hapa tutapata
picha halisi kwamba ni dhahiri Watanganyika
wanafaidika sana na hali hii iliopo hivi
sasa.Isitoshe Watanganyika mara zote hutoa vitisho kwamba pindipo Muungano ukivunjika basi
Zanzibar na hasa Wapemba ndio watakaoumia kwa
vile wamejiimarisha sana huko wamejenga
magorofa, hii inaonesha kwamba kuna lengo la
kuwafukuza Wazanzibar Tanganyika kama
kuwapa adhabu, watu wanasahau historia kwani Zanzibar baada ya Mapinduzi baadhi ya watu
walinyang’anywa majumba yao, mashamba na
vyenginevyo na hadi sasa watu wanaishi. Sasa huo
udugu unaozungumziwa na Watanganyika ndio
huo ? Jee wale Wazanzibar au Watanganyika
wanaoishi United kingdom,Canada,Marekani,Falme za kiarabu nao pia warejeshwe maanake hawa
wote hawakuungana na Nchi hizo, nako huko pia
wamejiimarisha hizo ni propaganda za kijinga na
ulimbukeni. Nashindwa kuelewa kuona Watu ambao wanajiita
Wasomi wa Watanzania wakiwemo ,
Marais,Mawaziri,Wabunge,Wawakilishi na
Waandishi wa habari wanashindwa kufahamu
maana ya Nchi kuwa huru,haki za
binaadamu,uhuru wa kuabudu,demokrasia ya kweli,usawa kwa wote, lakini pia dhana ya
Muuungano kwa Nchi husika ni nini. Naamini
wangalifahamu dhana hizi basi wangeliondokana
na zile kasumba na fikra za ukandamizaji
zilizoletwa na Wakoloni weupe na baadae
kurithishwa kwa Wakoloni weusi kama vile Mwalimu Nyerere na baadhi ya Viongozi wa Afrika
ambao kwao wao mabadiliko ya kidemokrasia ni
mwiko. Sisi kama kizazi kipya tunaenda kwa
misingi ya mabadiliko ya ulimwengu na
teknolojia,sasa yale mawazo ya vijiji vya ujamaa
watu kuishi maporini na Azimio la Arusha yamepitiwa na wakati lazima Serikali walielewe hilo. Nimekuwa nikishangaa sana kuona Serikali ya
Tanganyika inajaribu kufanya kila
inavyowezekana kujaribu kuzuia na kuzima wimbi
la Wazanzibar kupasua bahari na kuelekea Nchi
kavu,kuna haja ya kujiuliza kulikoni ? Jee hii ni haki
kwa nchi mbili zenye haki sawa na zilizoungana kwa hiari ?Mbona inaonekana zaidi kwamba Taifa
moja linalitawala jengine. Muungano huu
umekuwa ni ndoana kwa Wazanzibar na tusifikirie
kwamba ndoana hii kwa vile tumeshaimeza
tutakuwa salama hata tukiitoa basi lazima
tushikamane. Watanzania lazima tukubali kwamba mabadiliko katika Muungano huu ni jambo la
lazima kama kufa na mwanaadamu,tukidharau
basi tukubali kwamba madhara yake yatakuwa
makubwa kuliko faida yake. Wazanzibar wamechoka na utashi wa watu binafsi
kujiona kwamba Zanzibar ni miliki ya kikundi
fulani,watu fulani, chama fulani,fikra kama hizo
zitatufikisha pabaya. Leo hii imekuwa ni mazoea
kwa Serikali ya Tanganyika kuwanyanyasa
Wazanzibar kwa kutumia vitimba kwiri na Wahafidhina wa Kizanzibar waliopandikizwa
kuzima madai ya Wazanzibar kuhoji uhalali wa
Muungano.Imekuwa kama desturi kwa Viongozi
wa bara hasa wastaafu akina, Ali Hassan
Mwinyi,Benjamini mkapa kuingilia mambo ya ndani
ya Zanzibar lakini pia kuzidisha hasama miongoni mwa Wazanzibar, hali hii tutaenda nayo mpaka
lini.Sio kweli kwamba wanawapenda Wazanzibar
bali wanayafanya hayo kulinda maslahi yao
binafsi.Wakati umefika kuachiwa Wazanzibar
wajiamulie mambo yao wenyewe, na kuwa Taifa
huru,hivi Watanganyika wanaogopa nini ? Muungano huu umekuwa kama ni chaka ambalo
limeficha siri nzito,linalindwa kwa nguvu zote za
dola lakini kubwa zaidi ni kuona hata waandishi
wa habari kule bara wanashirikiana vizuri na
Serikali yao ili kuisadia kuwakandamiza
Wazanzibar kudai haki yao. Nimekuwepo Zanzibar kwa muda mrefu sasa, nimeona na kushuhudia
mengi yanayotokea hapa Zanzibar lakini takribani
waandishi wote wa habari wanashirikiana na
vyombo vya dola kuficha ukweli na kuzidi
kuwaona Wazanzibar kama vile ni maadui pale
wanapodai haki yao ya msingi ndani ya Muungano.Nilifikiria kuona kama vyombo vya
habari vitakuwa mstari wa mbele kufichua uovu
katika jamii yetu kinyume chake ndio wao
wanaoikandamiza Jamii yetu kwa fitna,uongo na
ubabaishaji wa habari na matukio ya kweli.Fahari
ya vyombo vya habari pamoja na waandishi waTanzania ni kutangaza propaganda za Serikali
na jinsi ya kuwadhibiti Wananchi ili waone kwamba
umaskini tulionao ndio maumbile yetu ,sasa hio
demokrasi inayozungumziwa na katiba mpya
inayotegemewa ipo wapi. Ukweli unafichwa na propaganda ndizo nyimbo za
Waandishi wa habari na baadhi yao tayari
wanafanya kazi ya serikali ya Tanganyika
kupotosha wananchi na ulimwengu kwa jumla
ukweli na uhalisia wake.Sasa taaluma hii ya
uandishi ina maana gani kwa Watanzania,ikiwa yale maovu yaliotawala kwenye jamii yanashindwa
kufichuliwa.Hii ni kutokana na serikali ya
Tanganyika kuwarubuni kwa nia ya kuendeleza
sera ambazo kwa ulimwengu huu tunaokwenda
nao hazikubaliki tena. Ingawaje Serikali ya Tanganyika imejipanga vizuri
kwa kupenyeza vibaraka wake ndani ya Zanzibar
ambao huwalai kwa madaraka baadhi ya Viongozi
ili iwe rahisi kwao kuwathibiti Wazanzibar ni vyema
baadhi viongozi hawa wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wakaelewa kwamba hivi sasa maji yameshamwagika,Wazanzibar wameshikamana
kudai haki yao na hapana budi kuungana nao ili
malengo ya Wazanzibar yafanikiwe kwa usalama
na amani bila ya kumwaga damu.Ule wakati wa
kugombea vyeo umeshapitiwa na wakati,huu nu
wakati wakuona Kwamba Jamhuri ya watu Wazanzibar kwanza,baadae ndio tuangalie utawala
na mstakabali wetu kwa pamoja. ZANZIBA KWANZA: source mzalendo.net
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment