Msanii Ben Pol, King Of Rnb amewataka mashabiki zake waachane na habari za mitandao na kuwataka wawe wavumilivu mpaka pale atakapofunguka live leo usiku kupitia EATv ambapo ataweka wazi mambo yake mengi pamoja na
kufuzungumzia jambo ambalo limefanya mashabiki wengi kuwa na sintofahamu juu yake na msanii Ali Kiba.
Jana kupitia mtandao wa twitter Ben Pol alimuuliza msanii Kiba swali hili "Bro @OfficialAliKiba mi naona kama unakuwa overrated halafu inakugharimu.. au Haikugharimu?" Alihoji Ben Pol
Lakini swali hili kwa baadhi ya mashabiki lilichukuliwa tofauti na baadhi ya mashabiki wa Alikiba walianza kumjia juu msanii huyo kwa maneno lakini leo Ben Pol atakuwepo katika Friday Night Live ya EATV ambapo atafunguka mengi juu ya muziki wake,.
Thursday, December 17, 2015
Ben Pal afunguka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment