Monday, August 13, 2012
Tanzania Vs Malawi
MGOGORO wa siku nyingi wa mpaka katika
Ziwa Nyasa baina ya Serikali ya Tanzania na
Malawi umeibuka kwa kasi baada ya kuwa
umetulia kwa muda mrefu.
Akiwa Bungeni hivi karibuni kuwasilisha
hotuba ya wizara yake kwa mwaka wa
fedha wa 2012/13, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania, Bw. Bernard Membe, aliionya nchi
ya Malawi kusitisha shughuli za utafiti wa
mafuta na gesi katika ziwa hilo.
"Serikali iko tayari kulinda mipaka kwa
gharama yoyote ile na inaitahadharisha
Serikali ya Malawi kuondoka mara moja na
kusitisha shughuli zozote zile za utafiti
ndani ya Ziwa Nyasa ndani ya nyuzi 11 hadi
9, kwani sehemu hiyo ni mali ya Tanzania,"
alisema Bw. Membe.
Bw.Membe aliongeza kuwa Tanzania
itakuwa tayari kutumia gharama zozote
kulinda mipaka yake na kuitaka Malawi
kuacha mara moja kuendelea kutoa vibali
kwa kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta
na gesi.
Eneo hilo la mwambao wa Ziwa Nyasa, Bw.
Membe alisema, linatumiwa na wakazi zaidi
600,000, ambao maisha yao ya kila siku
yanategemea ziwa hilo, hivyo kamwe
Serikali haitakubali kuona wananchi wake
wakinyanyasika.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa
Tanzania, Jaji Frederick Werema alinukuliwa
na 'Daily Times' la Malawi akimjibu Mbunge
wa Mbeya (Vitu Maalum), Bi. Hilda Ngoye,
akisema, ÒHatutaki Watanzania waombe
ruhusa kutoka Malawi kuchota maji au
kuvua Ziwa Nyasa. Kama hatufikii
makubaliano tunalipeleka suala hili kwenye
sheria za kimataifa.Ó
Bi. Ngoye alidai kwamba watalii wa Malawi
na boti za uvuvi zimekuwa zikiingia
kwenye eneo la maji ya Tanzania kadri
wanavyotaka.
âÓWatanzania wanaoishi kuzunguka Ziwa
Nyasa wanahaki ya kuvua na kufanya
shughuli nyingine za uzalishaji katika ziwa
hilo, bila kupewa vitisho,Ó Bi. Ngowe
aliliambia Bunge la Tanzania, akitaka
maelezo kutoka Serikalini kuhusu mpaka wa
Tanzania na Malawi.
Kwa upande wake, mwandishi Bw. Cedrick
Ngalande wa gazeti la 'Malawi Times' la
Agosti 6,2012 aliandika katika maoni yake
akidai kwamba wakati wa Uhuru watu
wachache nchini Tanzania walitaka kumega
sehemu kubwa ya Ziwa Malawi (Ziwa
Nyasa) kama wanavyoliita wenyewe.
Alisema wakati wa enzi za utawala wa Dkt
Kamuzu Banda, Tanzania haikuwahi
kuzungumzia wazo la kuligawa ziwa na
suala hilo lilikuwa karibu limesahaulika
kabisa wakati wa utawala wa Dkt. Bakili
Muluzi na hata baadaye.
Aliendelea kuhabarisha kwamba marehemu
Dkt. Bingu wa Mutharika aliipa jukumu
kampuni moja kuanza kazi ya utafutaji
mafuta katika ziwa hilo na Tanzania
haukusema lolote wakati huo na ndicho
chanzo cha kuibuka mgogoro huo.
"Sasa tuna Rais mpya na ghafla Watanzania
wanataka kwamba Serikali iache kufanya
shughuli zote za utafutaji mafuta katika
ziwa hili mpaka masuala yote
yanayohusiana na mipaka yametolewa
ufafanuzi. Kwa nini iwe sasa? Alihoji Bw.
Ngalande.
Bw. Ngalande alisema wakati Bi. Joyce
Banda alipotwaa madaraka ya urais,
ilionekana kwamba Malawi sasa itatekeleza
kila kitu anachoagizwa kufanya Bi. Banda
na Jumuiya ya Nchi Hisani.
Mwandishi huyo alisema baadhi ya
magazeti ya Uingereza yalishangazwa sana
na hali hiyo kiasi cha kuwaita watu wa
Malawi ÓTaifa linaloogopa wafadhiliÓ.
Alisema Rais Joyce Banda aliwahi kwenda
London na hata kumpigia magoti Malkia
Elizabeth, ambayo ni ishara ya ajabu sana
na ukitilia maanani wote wawili ni wakuu
wa nchi.
"Sawa, maneno yote haya na matendo
ukiyajumuisha pamoja yanatoa picha ya
uongozi dhaifu wa Malawi. Dunia imenusa
harufu ya damu. Sasa Tanzania imeamua ni
wakati wa kuligawa ziwa. Kumbuka
kwamba hawakulileta wazo hili wakati Bw.
Muluzi au Bw. Mutharika walipokuwa
madarakani," alisema Bw. Ngalande.
"Kama tutaipa Tanzania heshima kusikiliza
ombi lake, mtu atashangaa ni kitu gani
kitakachofuata baadaye. Je, sasa watadai
Chitipa (wilaya ya kaskazini mwa Malawi)?
Je, Msumbiji nayo itadai Mlima Mulanje ni wa
kwake? Bw. Ngalande aliendelea kuhoji.
"Serikali ni lazima iweke wazi kwamba
hakuna sehemu yoyote ya Malawi ifanyiwe
mjadala Òkwisha!Ó Sasa ni wakati wa
kuonesha uwezo wetu. Iambie Tanzania
kwamba Ziwa Malawi siku zote lilikuwa,
limekuwa na litakuwa la Malawi," aliandika
katika maoni yake.
"Cha kushangaza, baada ya maelezo yote
haya ya kiburi cha Serikali ya Tanzania, jibu
la Serikali yetu (Malawi) limekuwa hafifu.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje (Malawi)
ametoa kauli akisema suala hilo litatatuliwa
ÓkirafikiÓ.
"Kweli, Mhe. Waziri? Nini maana ya maelezo
ya kirafiki? Je, unapanga kuligawa ziwa na
kuipa heshima Tanzania kwa matakwa
yasiyokuwa na msingi? Utawezaje kuwa na
utatuzi wa amani kwa madai yasiyokuwa
ya msingi? Alihoji zaidi Bw. Ngalande.
Kwa upande wake, Bw. Patrick Kabambe,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi
za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Malawi alinukuliwa na gazeti la 'Daily Times'
la Malawi.
Bw. Kabambe alitoa kauli ya ajabu akisema,
ÒMadai yetu yako wazi juu ya suala hili.
Kwa mujibu wa makubalinano ya ecoland
1890 kati ya Serikali ya Uingereza na
Ujerumani, mpaka baina ya Malawi na
Tanzania ni kuanzia mwanzo wa maji ya
Ziwa Malawi upande wa Tanzania. Kwa hiyo,
tunalifahamu fika na tutaendelea kuihusisha
Tanzania kama majirani zetu wema.Ó
Mgogoro ni kuhusu nani anastahili hasa
kumiliki Ziwa Malawi kama linavyojulikana
na Wamalawi wengi na Lake Nyasa kama
linavyojulikana na Watanzania wengi.
Kwa mujibu wa Malawi, hili sio suala la
kufanyiwa mjadala. Malawi wakidai
wanamiliki asimia 100 ya Ziwa Malawi na
kama wataenda kwa mtazamo wa baba yao
wa taifa, Dkt. Hastings Kamuzu Banda,
Malawi kama ilivyokuwa ikijulikana, Maravi
Kingdom, inaweza kutanuka mpaka baadhi
ya maeneo ya Tanzania na hata Msumbiji.
Kwa mujibu wa Tanzania kwa upande
mwingine, ziwa hilo linatumiwa kwa
pamoja na mpaka wa nchi hizi mbili
unapaswa kufuata mstari wa 'median'
katika Ziwa Nyasa.
Huu ndio umekuwa msimamo wa Serikali ya
Tanzania na shughuli yoyote
itakayofanywa na Malawi kupita mstari huu
itachukuliwa kama Òkuingia eneo lisilo
lakeÓ.
Kihistoria mgogoro huu unaanzia Mkutano
wa Berlin na tatizo lipo kwenye Sheria ya
Bunge la Berlin ya 1885, iliyosainiwa na
mataifa 13 yenye nguvu ya Ulaya
yaliyohudhuria mkutano huo wa Kuigawa
Afrika.
Kinyang'anyiro cha kuigawa Afrika
Kwa mujibu wa hati za kugawa mpaka
kuzunguka Ziwa Nyasa na kusimamiwa na
mkataba wa nchi zinazozungumza lugha ya
Kiingereza na Ujerumani tarehe 1, Julai,
1890, Dkt Banda mwaka 1962 aliwahi kudai
kwamba sehemu moja ya Msumbiji ilipaswa
kuwa ya Malawi, wakati huo ikiitwa
Nyasaland.
Tanzania nayo inaweza kuonesha ramani
zinazoonesha mstari wa 'median' kama
mpaka na ramani hizo hazijawahi kwenda
kinyume na yaliyomo katika mkataba huo.
Mgogoro wa Ziwa Nyasa utakuwa vigumu
kufutika siku yoyote hivi karibuni kwa
pande zote mbili za Tanzania na Malawi na
kabla hata ya Uhuru.
Mtu anaweza kushangaa kama Watanzania
ni wendawazimu kudai nusu ya ukubwa wa
ziwa ambapo waliotengeneza ramani hizo
wanaonesha mstari wa 'median' kama
mpaka. Kuna baadhi ya mikataba ya
kimataifa inayoshughulika na haki
zinazohusiana na maji.
Kutokana na maelezo ya Bw. Patrick
Kabambe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wa Malawi, ufumbuzi wa suala hili bado ni
mgumu.
ÒBila shaka, tulifanya majadiliano ya mpaka
na tukawaambia Watanzania kwamba kwa
jinsi tunavyoelewa, ziwa lote ni mali ya
MalawiÓ alisema Bw. Kabambe.
Ushauri umetolewa kwamba pande zote
mbili za mgogoro huo zinapaswa kukutana
na kufikia makubaliano kwa amani.
Dkt. Hastings Kamuzu Banda aliwahi
kusema, Òsisi sote ni ndugu ramani na
mipaka tuliwekewa na wakoloni, kwa hiyo,
sisi sote (Wamalawi na Watanzania) tuvue
samaki na kuogelea pamoja katika ziwa zuri
la Nyasa."
Tanzania imekuwa na uzoefu mkubwa
ukilinganisha na Malawi katika medani za
kivita. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
limeshiriki mapigano mengi kwa mafanikio
makubwa ikiwemo oparesheni dhidi ya
wakoloni wa Kireno 1960 nchini Msumbiji.
Kama hiyo haitoshi, JWTZ iliwahi kupigana
dhidi ya majeshi ya Rhodesia na Afrika ya
Kusini (1975-1980) na dhidi ya magaidi wa
RENAMO wa Msumbiji 1986-1988.
JWTZ iliwahi pia kutoa kipigo kitakatifu
katika vita ya Kagera 1978 dhidi ya majeshi
ya nduli Iddi Amin wa Uganda, ambapo
nduli huyo aliweza kuitoroka nchi yake na
kuishi uhamishoni mpaka mauti
yalipomkuta.
JWTZ pia imeshiriki usimamizi wa kulinda
amani pamoja na Majeshi ya Umoja wa
Mataifa nchini Liberia, eneo la Darfur nchini
Sudan na nchi ya Lebanon.
No comments:
Post a Comment