Monday, August 13, 2012
Uraiqat ataka Palestinaitambuliwe rasmi UN
Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeitaka
jamii ya kimataifa kuunga mkono
uwanachama wa Palestina kama nchi huru
katika Umoja wa Mataifa. Saeb Uraiqat
kiongozi wa timu ya mazungumzo ya
Mamlaka ya Ndani ya Palestina leo ameitaka
jamii ya kimataifa kuunga mkono ombi
litakalowasilishwa tena na PLO, la kutaka
Palestina iwe nchi mwanachama
inayojitegemea katika Umoja wa Mataifa.
Huku akiashiria kwamba nchi nyingi za
Kiarabu na Kiislamu zinaunga mkono
kutambuliwa rasmi Palestina kama nchi
huru, Uraiqat amesisitiza kuwa, Mamlaka ya
Ndani ya Palestina itaendelea na jitihada
zake za kufanikisha suala hilo licha ya
mashinikizo mengi yanayoikabili. Mwaka
uliopita Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka
ya Ndani ya Palestina alitoa pendelezo la
kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina
kwa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa lakini kutokana na uungaji mkono
wa Marekani kwa Israel na ushawishi wa
tawala hizo kwenye umoja huo, pendekezo
hilo halikupitishwa.
No comments:
Post a Comment