Wednesday, August 15, 2012
China Bans Muslims from Fastingduring Ramadan
Beijing: China has banned Muslims in the
northwestern province of Xinjiang from
fasting during the month of Ramadan. The
government says the move is motivated by
health concerns, but others say it is a
campaign to secularize the Muslim minority
that can spread violence.
Guidance posted on several government
websites called on Communist Party leaders
to restrict Muslim civil servants, students
and teachers from observing fast, visiting
mosques and performing other relihious
activities during the holy month.
The statement posted on the Xinjiang
government website urged party leaders to
bring “gifts” of food to local village leaders
to ensure that they were eating during
Ramadan.
A statement from Zonglang township in
Xinjiang’s Kashgar district said that “the
county committee has issued
comprehensive policies on maintaining
social stability during the Ramadan period.
“It is forbidden for Communist Party cadres,
civil officials (including those who have
retired) and students to participate in
Ramadan religious activities,” said the
statement.
There is “a much more public and concerted
effort” than in previous years and in some
cases Communist Party leaders are
delivering food to village elders to try to get
them to break their fast, according to Dru
Gladney, a professor of anthropology at
Pomona College in California and an expert
on China’s Muslim minorities.
Regional spokeswoman Hou Hanmin was
quoted in the state-run Global Times
newspaper Friday as saying authorities
encourage people to “eat properly for study
and work” but don’t force anyone to eat
during Ramadan.
Xinjiang is home to about nine million
Uighurs, largely a Muslim ethnic minority,
many of whom accuse China’s leaders of
religious and political persecution. Long-
simmering resentment among Uighurs over
rule by China’s Han majority and an influx
of migrants has sporadically erupted into
deadly violence that claimed 200 lives in
July 2009.
World Uyghur Congress, an exiled rights
group, warned the policy would force “the
Uighur people to resist against the Chinese
rule even further.”
“By banning fasting during Ramadan, China
is using administrative methods to force the
Uighur people to eat in an effort to break
the fasting,” said Al-Jazeera has quoted
group spokesman Dilshat Rexit as saying.
Monday, August 13, 2012
Iran earthquake relief effortsbegin after 250 killed
Relief operations are under way in Iran
after two strong earthquakes in the north-
west left at least 250 people dead and
more than 2,000 injured.
The 6.4 and 6.3 quakes struck near Tabriz
and Ahar in in East Azerbaijan province on
Saturday afternoon, followed by dozens of
aftershocks.
More than 100 villages suffered damage -
thousands of people spent the night in
emergency shelters or in the open.
Relief agencies are providing survivors
with tents, bread and drinking water.
The BBC's Mohsen Asgari in the capital
Tehran says hundreds of people were
rescued overnight, but that the aftershocks
had made the operation exhausting.
By midday on Sunday, Deputy Interior
Minister Hassan Ghadami said that "all those
under debris have been rescued and the
quake-stricken people are now being
provided with their basic needs".
Our correspondent says the operation could
be completely quickly because villagers
knew each other well so knew where to
search, and because the houses were small.
'Mass grave'
The towns of Haris and Varzaqan were also
among those hit and one resident of Tabriz
told the BBC: "The quake has created huge
panic among the people. Everyone has
rushed to the streets."
But local officials said all the deaths have
been in rural areas, not in the main towns
and cities.
The official Fars news agency reported that
about 110 villages had been damaged. At
least were four totally flattened and 60
others sustained extensive damage.
"This village is a mass grave," said Alireza
Haidaree, who had been searching for
survivors in Baje Baj village.
"There are so many other villages that have
been completely destroyed," he told AFP.
Reports said rescuers attempting to contact
remote villages had to do so by radio as
many phone lines were cut off.
Uraiqat ataka Palestinaitambuliwe rasmi UN
Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeitaka
jamii ya kimataifa kuunga mkono
uwanachama wa Palestina kama nchi huru
katika Umoja wa Mataifa. Saeb Uraiqat
kiongozi wa timu ya mazungumzo ya
Mamlaka ya Ndani ya Palestina leo ameitaka
jamii ya kimataifa kuunga mkono ombi
litakalowasilishwa tena na PLO, la kutaka
Palestina iwe nchi mwanachama
inayojitegemea katika Umoja wa Mataifa.
Huku akiashiria kwamba nchi nyingi za
Kiarabu na Kiislamu zinaunga mkono
kutambuliwa rasmi Palestina kama nchi
huru, Uraiqat amesisitiza kuwa, Mamlaka ya
Ndani ya Palestina itaendelea na jitihada
zake za kufanikisha suala hilo licha ya
mashinikizo mengi yanayoikabili. Mwaka
uliopita Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka
ya Ndani ya Palestina alitoa pendelezo la
kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina
kwa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa lakini kutokana na uungaji mkono
wa Marekani kwa Israel na ushawishi wa
tawala hizo kwenye umoja huo, pendekezo
hilo halikupitishwa.
Tanzania Vs Malawi
MGOGORO wa siku nyingi wa mpaka katika
Ziwa Nyasa baina ya Serikali ya Tanzania na
Malawi umeibuka kwa kasi baada ya kuwa
umetulia kwa muda mrefu.
Akiwa Bungeni hivi karibuni kuwasilisha
hotuba ya wizara yake kwa mwaka wa
fedha wa 2012/13, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania, Bw. Bernard Membe, aliionya nchi
ya Malawi kusitisha shughuli za utafiti wa
mafuta na gesi katika ziwa hilo.
"Serikali iko tayari kulinda mipaka kwa
gharama yoyote ile na inaitahadharisha
Serikali ya Malawi kuondoka mara moja na
kusitisha shughuli zozote zile za utafiti
ndani ya Ziwa Nyasa ndani ya nyuzi 11 hadi
9, kwani sehemu hiyo ni mali ya Tanzania,"
alisema Bw. Membe.
Bw.Membe aliongeza kuwa Tanzania
itakuwa tayari kutumia gharama zozote
kulinda mipaka yake na kuitaka Malawi
kuacha mara moja kuendelea kutoa vibali
kwa kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta
na gesi.
Eneo hilo la mwambao wa Ziwa Nyasa, Bw.
Membe alisema, linatumiwa na wakazi zaidi
600,000, ambao maisha yao ya kila siku
yanategemea ziwa hilo, hivyo kamwe
Serikali haitakubali kuona wananchi wake
wakinyanyasika.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa
Tanzania, Jaji Frederick Werema alinukuliwa
na 'Daily Times' la Malawi akimjibu Mbunge
wa Mbeya (Vitu Maalum), Bi. Hilda Ngoye,
akisema, ÒHatutaki Watanzania waombe
ruhusa kutoka Malawi kuchota maji au
kuvua Ziwa Nyasa. Kama hatufikii
makubaliano tunalipeleka suala hili kwenye
sheria za kimataifa.Ó
Bi. Ngoye alidai kwamba watalii wa Malawi
na boti za uvuvi zimekuwa zikiingia
kwenye eneo la maji ya Tanzania kadri
wanavyotaka.
âÓWatanzania wanaoishi kuzunguka Ziwa
Nyasa wanahaki ya kuvua na kufanya
shughuli nyingine za uzalishaji katika ziwa
hilo, bila kupewa vitisho,Ó Bi. Ngowe
aliliambia Bunge la Tanzania, akitaka
maelezo kutoka Serikalini kuhusu mpaka wa
Tanzania na Malawi.
Kwa upande wake, mwandishi Bw. Cedrick
Ngalande wa gazeti la 'Malawi Times' la
Agosti 6,2012 aliandika katika maoni yake
akidai kwamba wakati wa Uhuru watu
wachache nchini Tanzania walitaka kumega
sehemu kubwa ya Ziwa Malawi (Ziwa
Nyasa) kama wanavyoliita wenyewe.
Alisema wakati wa enzi za utawala wa Dkt
Kamuzu Banda, Tanzania haikuwahi
kuzungumzia wazo la kuligawa ziwa na
suala hilo lilikuwa karibu limesahaulika
kabisa wakati wa utawala wa Dkt. Bakili
Muluzi na hata baadaye.
Aliendelea kuhabarisha kwamba marehemu
Dkt. Bingu wa Mutharika aliipa jukumu
kampuni moja kuanza kazi ya utafutaji
mafuta katika ziwa hilo na Tanzania
haukusema lolote wakati huo na ndicho
chanzo cha kuibuka mgogoro huo.
"Sasa tuna Rais mpya na ghafla Watanzania
wanataka kwamba Serikali iache kufanya
shughuli zote za utafutaji mafuta katika
ziwa hili mpaka masuala yote
yanayohusiana na mipaka yametolewa
ufafanuzi. Kwa nini iwe sasa? Alihoji Bw.
Ngalande.
Bw. Ngalande alisema wakati Bi. Joyce
Banda alipotwaa madaraka ya urais,
ilionekana kwamba Malawi sasa itatekeleza
kila kitu anachoagizwa kufanya Bi. Banda
na Jumuiya ya Nchi Hisani.
Mwandishi huyo alisema baadhi ya
magazeti ya Uingereza yalishangazwa sana
na hali hiyo kiasi cha kuwaita watu wa
Malawi ÓTaifa linaloogopa wafadhiliÓ.
Alisema Rais Joyce Banda aliwahi kwenda
London na hata kumpigia magoti Malkia
Elizabeth, ambayo ni ishara ya ajabu sana
na ukitilia maanani wote wawili ni wakuu
wa nchi.
"Sawa, maneno yote haya na matendo
ukiyajumuisha pamoja yanatoa picha ya
uongozi dhaifu wa Malawi. Dunia imenusa
harufu ya damu. Sasa Tanzania imeamua ni
wakati wa kuligawa ziwa. Kumbuka
kwamba hawakulileta wazo hili wakati Bw.
Muluzi au Bw. Mutharika walipokuwa
madarakani," alisema Bw. Ngalande.
"Kama tutaipa Tanzania heshima kusikiliza
ombi lake, mtu atashangaa ni kitu gani
kitakachofuata baadaye. Je, sasa watadai
Chitipa (wilaya ya kaskazini mwa Malawi)?
Je, Msumbiji nayo itadai Mlima Mulanje ni wa
kwake? Bw. Ngalande aliendelea kuhoji.
"Serikali ni lazima iweke wazi kwamba
hakuna sehemu yoyote ya Malawi ifanyiwe
mjadala Òkwisha!Ó Sasa ni wakati wa
kuonesha uwezo wetu. Iambie Tanzania
kwamba Ziwa Malawi siku zote lilikuwa,
limekuwa na litakuwa la Malawi," aliandika
katika maoni yake.
"Cha kushangaza, baada ya maelezo yote
haya ya kiburi cha Serikali ya Tanzania, jibu
la Serikali yetu (Malawi) limekuwa hafifu.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje (Malawi)
ametoa kauli akisema suala hilo litatatuliwa
ÓkirafikiÓ.
"Kweli, Mhe. Waziri? Nini maana ya maelezo
ya kirafiki? Je, unapanga kuligawa ziwa na
kuipa heshima Tanzania kwa matakwa
yasiyokuwa na msingi? Utawezaje kuwa na
utatuzi wa amani kwa madai yasiyokuwa
ya msingi? Alihoji zaidi Bw. Ngalande.
Kwa upande wake, Bw. Patrick Kabambe,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi
za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Malawi alinukuliwa na gazeti la 'Daily Times'
la Malawi.
Bw. Kabambe alitoa kauli ya ajabu akisema,
ÒMadai yetu yako wazi juu ya suala hili.
Kwa mujibu wa makubalinano ya ecoland
1890 kati ya Serikali ya Uingereza na
Ujerumani, mpaka baina ya Malawi na
Tanzania ni kuanzia mwanzo wa maji ya
Ziwa Malawi upande wa Tanzania. Kwa hiyo,
tunalifahamu fika na tutaendelea kuihusisha
Tanzania kama majirani zetu wema.Ó
Mgogoro ni kuhusu nani anastahili hasa
kumiliki Ziwa Malawi kama linavyojulikana
na Wamalawi wengi na Lake Nyasa kama
linavyojulikana na Watanzania wengi.
Kwa mujibu wa Malawi, hili sio suala la
kufanyiwa mjadala. Malawi wakidai
wanamiliki asimia 100 ya Ziwa Malawi na
kama wataenda kwa mtazamo wa baba yao
wa taifa, Dkt. Hastings Kamuzu Banda,
Malawi kama ilivyokuwa ikijulikana, Maravi
Kingdom, inaweza kutanuka mpaka baadhi
ya maeneo ya Tanzania na hata Msumbiji.
Kwa mujibu wa Tanzania kwa upande
mwingine, ziwa hilo linatumiwa kwa
pamoja na mpaka wa nchi hizi mbili
unapaswa kufuata mstari wa 'median'
katika Ziwa Nyasa.
Huu ndio umekuwa msimamo wa Serikali ya
Tanzania na shughuli yoyote
itakayofanywa na Malawi kupita mstari huu
itachukuliwa kama Òkuingia eneo lisilo
lakeÓ.
Kihistoria mgogoro huu unaanzia Mkutano
wa Berlin na tatizo lipo kwenye Sheria ya
Bunge la Berlin ya 1885, iliyosainiwa na
mataifa 13 yenye nguvu ya Ulaya
yaliyohudhuria mkutano huo wa Kuigawa
Afrika.
Kinyang'anyiro cha kuigawa Afrika
Kwa mujibu wa hati za kugawa mpaka
kuzunguka Ziwa Nyasa na kusimamiwa na
mkataba wa nchi zinazozungumza lugha ya
Kiingereza na Ujerumani tarehe 1, Julai,
1890, Dkt Banda mwaka 1962 aliwahi kudai
kwamba sehemu moja ya Msumbiji ilipaswa
kuwa ya Malawi, wakati huo ikiitwa
Nyasaland.
Tanzania nayo inaweza kuonesha ramani
zinazoonesha mstari wa 'median' kama
mpaka na ramani hizo hazijawahi kwenda
kinyume na yaliyomo katika mkataba huo.
Mgogoro wa Ziwa Nyasa utakuwa vigumu
kufutika siku yoyote hivi karibuni kwa
pande zote mbili za Tanzania na Malawi na
kabla hata ya Uhuru.
Mtu anaweza kushangaa kama Watanzania
ni wendawazimu kudai nusu ya ukubwa wa
ziwa ambapo waliotengeneza ramani hizo
wanaonesha mstari wa 'median' kama
mpaka. Kuna baadhi ya mikataba ya
kimataifa inayoshughulika na haki
zinazohusiana na maji.
Kutokana na maelezo ya Bw. Patrick
Kabambe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wa Malawi, ufumbuzi wa suala hili bado ni
mgumu.
ÒBila shaka, tulifanya majadiliano ya mpaka
na tukawaambia Watanzania kwamba kwa
jinsi tunavyoelewa, ziwa lote ni mali ya
MalawiÓ alisema Bw. Kabambe.
Ushauri umetolewa kwamba pande zote
mbili za mgogoro huo zinapaswa kukutana
na kufikia makubaliano kwa amani.
Dkt. Hastings Kamuzu Banda aliwahi
kusema, Òsisi sote ni ndugu ramani na
mipaka tuliwekewa na wakoloni, kwa hiyo,
sisi sote (Wamalawi na Watanzania) tuvue
samaki na kuogelea pamoja katika ziwa zuri
la Nyasa."
Tanzania imekuwa na uzoefu mkubwa
ukilinganisha na Malawi katika medani za
kivita. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
limeshiriki mapigano mengi kwa mafanikio
makubwa ikiwemo oparesheni dhidi ya
wakoloni wa Kireno 1960 nchini Msumbiji.
Kama hiyo haitoshi, JWTZ iliwahi kupigana
dhidi ya majeshi ya Rhodesia na Afrika ya
Kusini (1975-1980) na dhidi ya magaidi wa
RENAMO wa Msumbiji 1986-1988.
JWTZ iliwahi pia kutoa kipigo kitakatifu
katika vita ya Kagera 1978 dhidi ya majeshi
ya nduli Iddi Amin wa Uganda, ambapo
nduli huyo aliweza kuitoroka nchi yake na
kuishi uhamishoni mpaka mauti
yalipomkuta.
JWTZ pia imeshiriki usimamizi wa kulinda
amani pamoja na Majeshi ya Umoja wa
Mataifa nchini Liberia, eneo la Darfur nchini
Sudan na nchi ya Lebanon.
Sunday, August 12, 2012
ULIMBOKA AREJEA NCHINI AKIWA FITI
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari, Dk
Steven Ulimboka amerejea nchini jana
akitokea Afrika Kusini alikopelekwa kwa
matibabu na kusema amepona kabisa.
Ulimboka, ambaye alikuwa anaratibu
migomo ya madaktari iliyofanyika mara
mbili mfululizo, alitekwa na watu
wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatano
ya Juni 27, mwaka huu na kupelekwa katika
msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam, ambako aliteswa na kujeruhiwa
vibaya.
Katika tukio hilo, daktari huyo aling’olewa
meno mawili na kucha za mkono mmoja na
baadaye kulazwa katika Kitengo cha
Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu
(ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI) katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, Juni
30, mwaka huu, alisafirishwa kwenda Afrika
Kusini kwa ajili ya vipimo na matibabu.
Dk Ulimboka aliwasili jana saa nane mchana
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA), akitembea mwenyewe
na kulakiwa na mamia ya wananchi wa Jiji
la Dar es Salaam, wakiwamo madaktari
wenzake pamoja na wanaharakati.
Huku akibubujikwa na machozi pamoja na
ndugu zake, madaktari na wanaharakati
nao walimpokea kwa machozi kisha
walimkinga kiasi ambacho kulitokea vurugu
za kila mmoja kutaka kumwona.
Akizungumza kwa ujasiri huku akizongwa
na madaktari pamoja na wanahabari,
Ulimbona alianza kwa kuwashukuru wote
waliofika kumpokea na pia kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kufikisha katika hali
aliyonayo sasa pamoja na Chama cha
Madaktari waliosaidia kupata fedha za
matibabu.
Alisema kwa sasa afya yake imeimarika na
amepona kabisa na yuko tayari kufanya
jambo lolote bila utata na kuruhusu maswali
kwa wanahabari, lakini madaktari wenzake
walikataa na kumtaka aende kwenye gari ili
aondoke kwenda kupumzika. Alitii agizo hilo
na kuondoka kwenda kwenye gari.
Awali, kabla Dk Ulimboka hajawasili JNIA, nje
ya uwanja wa ndege madaktari pamoja na
wanaharakati walisikika wakiimba nyimbo
mbalimbali zikiwamo za ‘Tanzania
Nakupenda, ‘Kama siyo juhudi zako Nyerere’
pamoja na kuhamasishana kuwa Solidarity
Forever (Mshikamano Daima).
Baada ya kutembea hatua chache na kufika
lilipokuwa gari lililombeba, Dk Ulimboka
alisimama na kutaka kuzungumza jambo na
wanahabari, lakini madaktari na nduguze
walimkataza tena na kudai wamuache ili
aende kupumzika.
Katibu wa Jumuiya hiyo ya Madaktari, Dk
Edwin Chitage akizungumzia gharama za
matibabu ya Dk Ulimboka, alisema
wanazikusanya na kujumlisha na
watazieleza hivi karibuni kwa vyombo vya
habari.
Wanaharakati waliokuwapo uwanjani hapo,
walizungumzia kurejea kwa Dk Ulimboka na
kudai mapambano yameanza upya, kwani
kilichomfanya daktari huyo kupigwa ni
kupigania maslahi ya Watanzania wote.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari
Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya alisema
umefika wakati wa Watanzania kusimama
na kuacha woga na unafiki katika kupigania
haki za afya zao.
Nkya alisisitiza kuwa mapambano
aliyoyaanzisha Dk Ulimboka yanaendelea.
Jambo lililoungwa mkono na Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP, Usu Malya alisema
mapambano ya Dk Ulimboka ni ya
Watanzania wote, hivyo kila mmoja
anatakiwa kumuunga mkono.
Dk Ulimboka alitekwa na kuumizwa vibaya
wakati mgomo wa madaktari nchini ukiwa
unaendelea, na tangu wakati huo baadhi ya
wanasiasa hasa wa upinzani, na
wanaharakati wamekuwa wakiituhumu
Serikali kuhusika katika kutekwa na
kupigwa kwa daktari huyo.
Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Rais Jakaya
Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
mara kadhaa baada ya tukio hilo, imesisitiza
kuwa haihusiki na unyama huo, na wala
haikuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Tayari raia wa Kenya, Joshua Mulundi (21)
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akituhumiwa
kumteka na kufanya jaribio la kumwua Dk
Ulimboka.
MJUSI ALIYEPELEKWA UJERUMANI KUREJESHWA NCHINI
SERIKALI ina mpango wa kumrudisha nchini
mjusi maarufu aina ya Dinosaur
aliyechukuliwa mkoani Lindi zaidi ya miaka
100 iliyopita na kupelekwa Ujerumani
anakokadiriwa kuiingizia nchi hiyo zaidi ya
Dola za Marekani bilioni tatu kwa mwaka,
sawa na karibu Sh trilioni tano.
Hayo yalisemwa bungeni juzi na Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
alipozungumzia mikakati ya serikali katika
kukuza utalii nchini. Nyalandu alisema
Serikali itazungumza na Serikali ya
Ujerumani juu ya suala hilo na kwamba,
kama atarudishwa, atapelekwa mkoani
Lindi.
Aidha, alisema kama hilo litashindikana
wataangalia pia uwezekano wa kupata
asilimia fulani ya fedha inayotokana na
watalii wanaomiminika kumuona mjusi
huyo.
“Katika mambo ya Kale, kuna hili la Mjusi
wetu maarufu kama Dinasour ambaye
taarifa tulizonazo anaipatia Ujerumani dola
bilioni tatu kwa mwaka… huyu alichukuliwa
Lindi na wakoloni wa Ujerumani
akapelekwa iliyokuwa Berlin Mashariki…
tunataka tumrudishe nchini, tutazungumza
na Ujerumani… “Lakini niwahakikishie
wabunge na Watanzania, tutawashirikisha
wadau ili tujue sera na mtazamo wetu kama
taifa kuona tutakavyoamua kuzungumza na
Ujerumani tuamue kuomba mjusi wetu
arudi tumweke Lindi au abaki huko huko,
lakini tugawane mapato,” alisema.
Masalia ya mifupa ya mjusi huyo,
yalipatikana mwaka 1912 huko Tendaguru,
Kata ya Mipango katika Jimbo la Mchinga,
mkoani Lindi. Amehifadhiwa katika
Makumbusho ya Humbolt huko Ujerumani.
Nyalandu alikiri kuwapo kwa changamoto
nyingi katika kukuza utalii, lakini Serikali
imejipanga kufanya kazi kwa kasi ili
kuhakikisha yanafanyika mapinduzi
makubwa katika sekta ya utalii ili
ulinufaishe taifa.
Alisema “Hali ya utalii nchini hairidhishi na
wizara yangu imeazimia kufanya
mabadiliko makubwa. Nchi yetu inapata
watalii wachache tofauti na fursa
tulizonazo. Dhamira ya Serikali ni kuona nchi
inapata watalii milioni mbili kwa mwaka
ifikapo mwaka 2015. Kwa sasa, watalii
hawafiki milioni moja kwa mwaka.”
Alisema mikakati hiyo itakwenda sambamba
na kuongeza kasi ya ujenzi wa hoteli na
nyumba za kulala wageni ili kuwa na
uhakika wageni watakaokuja nchini
hawakosi makazi.
Nyalandu alisema mikakati pia inafanywa
kuboresha mazingira ya viwanja vya
ndege, akitolea mfano Uwanja wa Ndege
wa Mwanza utapandishwa hadhi na
mpango wa kuufanya kuwa wa kimataifa
zaidi, utabadilishwa jina na kuitwa Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti.
Waislamu wa Myanmar wazidikuteseka
Ripoti mbalimbali kutoka Myanmar
zinasema kuwa maafa makubwa yanatokea
katika kambi ya wakimbizi wa Kiislamu
katika jimbo la Rakhine. Kanali ya televisheni
ya Press imeripoti kuwa watu karibu 20
wakiwemo watoto wadogo wamefariki
dunia katika kambi hiyo ya Waislamu wa
jamii ya Rohingya huko Myanmar kutokana
na ukosefu wa dawa na chakula. Ripoti hiyo
inasema vijiji kadhaa vya Waislamu wa
kaskazini magharibi mwa Myanmar
vimeteketezwa kwa moto na Mabudha
wanaosaidiwa na jeshi la polisi, na wakazi
wa vijiji hivyo wamelazimika kuwa
wakimbizi. Mabudha hao wenye misimamo
mikali pia wamechoma moto misikiti
kadhaa. Umoja wa Mataifa umesema kuwa
ukatili wanaofanyiwa Waislamu wa
Myanmar ndiyo mkubwa zaidi kuwahi
kushuhudiwa duniani katika siku za hivi
karibuni. Shirika la Kutetea Haki za
Binadamu la Human Rights Watch (HRW)
limesema kuwa jeshi la Myanmar limetenda
jinai nyingi dhidi ya Waislamu wa Rohingya
walio wachache. Ripoti hiyo imefafanua
kuwa miongoni mwa jinai hizo ni kubakwa
wanawake wa jamii hiyo ya Waislamu
kaskazini mwa Myanmar.
Wakenya 13 wafariki dunia katika ajali ya mabasi ilotokea tanzania
Idadi ya watu walofariki katika ajali ya
mabasi mawili karibu na mji wa Tanga
Tanzania Ijuma asubuhi imefikia 13. Watu
42 wamejeruhiwa miongoni mwao 14
wako katika hali tabani, watu 29
hawakujeruhiwa.
Walofariki ni miongoni mwa kundi la
wanawake wa Kenya kutoka kanisa la
Presbyterian Church of East Africa - PCEA
kutoka Thika walokuwa wanasafiri kuelekea
Dar es Salaam kwa sherehe za kidini
Tanzania.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani
Tanzania, Ernest Mangu ameiambia sauti ya
Amerika kwamba serikali ya Kenya
inashirikiana kwa karibu sana na Tanzania
na imepeleka ndege maalum kuwasafirisha
nyumbani walonusurika.
MISRI YATUMA VIKOSI VYAKE SINAI
Misri imetumia Helicopter kufanya
mashambulizi ya mizinga dhidi ya
wakereketwa wenye imani kali walio
katika eneo la Sinai tangu mwaka
1973 katika kile jeshi la Misri
lililochotaja kama shambulio la
kurejesha utulivu.
Matumizi ya anga ni ishara ya
mabadiliko ya vita vya Misri dhidi ya
wakereketwa wa Kiislam ambao
wamezidisha shughuli zao katika
eneo lenye milima na jangwa lenye
mpaka na Israili na Gaza.
Mapema wiki hii wapiganaji
wakereketwa waliishangaza Misri
kwa ujasiri wao kwa shambulizi
ambamo askari 16 waliuawa, magari
ya jeshi yakaibwa na kuelekea Israel
kwa lengo la kujaribu kufanya
shambulio jingine.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye
televisheni ya taifa jeshi limesema
kua limeanzisha operesheni ya
mchanganyiko wa vikosi kwa kutaka
kurejesha utulivu huko Sinai, majeshi
yakiungwa mkono na Jeshi la anga.
Shambulio la siku ya jumapili ndio
baya kuwahi kufanywa huko Sinai
kwa miaka mingi na hatari kuliko
yote dhidi ya vikosi vya Misri
ikiashiria ongezeko la vitendo
vinavyokiukaq sheria katika eneo
hilo.
Katika tukio la hivi karibuni, watu
wenye silaha waliwafyatulia risasi
walinzi kwenye vizuizi huko El -arish,
mji mkuu wa Wilaya ya Sinai, mji ulio
umballi wa kilomota 50 kutoka
mpaka wa Gaza na Israili.
Ghasia kwenye mpaka wa Israel na
Misri inaweza kutishia mkataba wa
amani baina ya nchi hizi mbili.
Hio ndio sababu Israel imeiambia
Misri ichukue hatua za kusuluhisha
vurugu badala yake kupeleka vikosi
vyake. Israel imekubali kuondoa
baadhi ya masharti yanayozuwia
shughuli za kijeshi katika Sinai ili Wa
Misri waweze kuingiza vikosi zaidi.
Lakini uvamizi wa Misri dhidi ya kile
walichokiita magaidi hautobadili
lolote katika sehemu ya Sinai
inayokaliwa na makabilia ya Wa
Bedwini wenye fikra huria.
Ni eneo linalovutia kwa makundi
ambayo yangependa kutumia
sehemu isiyokua na utaratibu
wowote wa uongozi kwa aijili ya
kuifika Israili.Rais wa Misri
Mohammad Mursi aliahidi kwamba
atadhibiti eneo la Sinai kwa
ukamilifu.
Wednesday, August 8, 2012
Amnesty Internationallazionya pande zinazopiganakwenye mji wa Aleppo nchiniSyria kuacha kutumia silahanzito dhidi ya raia
Shirika la kimataifa la kutetea haki za
binadamu duniani la Amnesty
International limeonya dhidi ya
kuendelea kutumika kwa silaha nzito
kwenye mji wa Aleppo kati ya wanajeshi
wa Serikali na waasi wa jeshi huru la
Syria.
Picha mpya za satelite zimeonesha
kuongezeka kwa matumizi makubwa ya
silaha nzito kwenye mji wa Aleppo na
kuendelea kuzusha hofu kuhusu hali ya
usalama wa wananchi ambao wamenaswa
kwenye mji huo.
Wanaharakati nchini humo wamedai kuwa
wamegundua zaidi ya mashimo makubwa
600 yanayoonekana kwenye mji wa Aleppo
yamesababishwa na kutumika kwa silaha
nzito kwenye makazi.
Shirika la Amnesty International limesema
kuwa pande zote mbili zinazopigana
kwenye mji huo zinawajibika kutokana na
kile kinachoshuhudiwa na matatizo ambayo
wananchi wanakumbana nayo wakati
mapigano hayo yakiendelea.
Hapo jana waangalizi wa Umoja wa Mataifa
UN waliamua kuondoka kwenye mji huo
kwasababu za kiusalama baada ya
kuongezeka kwa mashambulizi ya anga
yanayofanywa na majeshi ya Syria.
Juma hili ujumbe maalumu wa Iran
umesafiri hadi mjini Damascus kukutana na
rais Bashar al-Asad, ujumbe ulioongozwa na
mpatanishi wake Saeed Jalili ambaye
anakutana kwa mara ya pili na utawala wa
Syria.
Ujumbe huo uko nchini Syria kujaribu
kushawishi kundi ambalo linawashikilia raia
wake zaidi ya 48 ambao liliwateka jumapili
iliyopita wakiwa njiani kuelekea uwanja wa
ndege.
Waasi wa Syria wamekuwa wakiituhumu
Serikali ya Iran kwa kuendelea kuiunga
mkono serikali ya Asad ambayo wamedai ni
haramu na katili kwa kuendelea kuwaua
wananchi wasio na hatia.
Hii leo waziri wa mambo ya nchi za nje wa
Iran Ali Akbar Salehi amesema miongoni
mwa raia wake waliotekwa mmoja kati yao
ni mwanajeshi mstaafu wa jeshi la nchi
hiyo.
Marekani yataka Rwanda kusitisha Msaada kwa Waasi wa M23
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
Hillary Clinton ameitaka serikali ya
Rwanda kuisaidia Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo DRC
kuwanyang'anya silaha waasi wa M23
na kusitisha msaada kwa Kundi hilo kwa
lengo la kupata suluhu ya mgogoro wa
Mashariki mwa nchi hiyo.
Clinton amesema wanataka kuona nchi za
Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR zinashiriki
kikamilifu katika kurejesha usalama nchini
DRC na kulisambaratisha Kundi la Waasi la
M23 ambalo linatekeleza mashambulizi
Mashariki mwa nchi hiyo.
Kauli hii inakuja kipindi hiki ambacho
Viongozi kutoka nchi kumi na moja za
Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiwa
kwenye mkutano wa siku mbili nchini
Uganda kujadili usalama wa DRC ili
kulimaliza Kundi la M23.
Clinton ametaka Viongozi hao wa Ukanda
wa Maziwa Makuu kutathimini kwa kina
namna ya kuweza kushughulikia mgogoro
huo na hatimaye kurejesha utulivu ambao
umepotea Mashariki mwa DRC.
Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa
Makuu ICGLR umeingia siku ya pili ambapo
Rais wa DRC Joseph Kabila Kabange
hatukutana tena na Rais wa Rwanda Paul
Kagame kama ambavyo ilipangwa awali na
badala yake wataandaliwa kikao chao
pekee.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Oriem
Okello amesema Viongozi hao wawili
hatokutana na badala yake Rais Yoweri
Kaguta Museveni ataandaa mkutano baina
yao na kwa sasa wamejiegemeza kujadili
kupata Jeshi litakalolinda amani mpaka mwa
DRC.
Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu ICGLR
wataamua Kikosi ambacho kitaenda kulinda
mipaka ya DRC na kukabiliana na uasi
ambao unafanywa na Kundi la Waasi la M23
ili kusaidia juhudi za amani.
DRC yenyewe imeshaainisha haitaki nchi ya
Rwanda ishirikishwe kwenye Jeshi hilo
kutokana na kudaiwa kuwafadhili Waasi wa
M23 huku Kigali yenyewe ikishinikiza
inataka kushiriki kwenye mpango wa
kurejesga amani.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Shirika la
Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa
OCHA Valerie Amos anaendelea na ziara yake
kuangalia madhara ya mashambulizi ya
Kundi la M23 nchini DRC.
Amos amesema hali ni mbaya Jimboni Kivu
kitu ambacho kama hakijadhibitiwa
kinaweza kuzua maafa zaidi kwa wananchi
wa eneo hilo kutokana na mashambulizi ya
mara kwa mara ambayo yamekuwa
yakifanywa na Kundi la Waasi la M23.
Kundi la Waasi la M23 limeendelea
kujigamba kupiga hatua kwenye
mapambano yake na Jeshi la Serikali hasa
katika maeneo ya Rutchuru na sasa
wanaendelea kusaka uungwaji mkono
kutoka kwa wananchi.
Tuesday, August 7, 2012
MALAWI Vs TANGANYIKA( TANZANIA BARA )
Malawi imekataa kuitikia wito wa
Tanzania kutaka isimamishe shughuli
za kutafuta mafuta na gesi ziwa
Malawi, wakati suluhu ya mvutano
wa mpaka ikisubiriwa.
Mvutano wa maneno umezuka kati
ya nchi hizo mbili baada ya Malawi
kuipa leseni Kampuni ya Uingereza
kufanya utafiti katika eneo hilo.
Maafisa nchini Tanzania wanasema
mvutano huo uliodumu kwa miaka
50 sasa unaweza kuwa mkubwa
iwapo ugunduzi wa mafuta na gesi
utatokea kwenye ziwa hilo
linalojulikana kama Ziwa Nyasa
nchini Tanzania.
Tanzania inasema inaendelea
kufanya mazungumzo na Malawi na
iko Tayari kulipeleka suala hilo
kwenye vyombo vya upatanishi.
"Hili ni suala nyeti sana na
tungependa litatuliwe kwa
maelewano, tutaendelea na
mazungumzo," Waziri wa Mambo ya
Nje wa Tanzania alisema.
Membe wiki iliyopita alviambia
vyombo vya habari nchini humo
kuwa "shughuli za uchimbaji katika
eneo la kaskazini mashariki mwa
ziwa hazina budi kusitishwa kupisha
mazungumzo kutatua mzozo huo
yafanyike."
Malawi, koloni la zamani la Uingereza,
kwa upande wake iliapa kuendelea
na chughuli za utafiti wa hewa gesi
mkaa (hydrocarbons).
Tanzania,lililotawaliwa na Ujerumani
na baadaye Uingereza, inadai kuwa
sehemu ya kilometa za mraba
29,600 sawa na maili 11,400 za ziwa,
wakati Malawi inarejea makubaliano
ya mwaka 1890 yanaonyesha kuwa
mpaka kati ya nchi hizo mbili uko
kwenye ufukwe upande wa
Tanzania.
Msumbiji pia inadai ina sehemu yake
katika ziwa hilo la tatu kwa ukubwa
barani Afrika.Mwezi Septemba
mwaka jana serikali ya marehemu
Bingu wa iliipa leseni kampuni ya
Surestream Petroleum, kutafiti
mafuta na gesi ziwani.
Mataifa hayo mawili yatafanya
mazungumzo juu ya mpaka
kaskazini mwa Malawi katika mji wa
Mzuzu Agosti 20 mwaka huu.
Iran Says Test of Upgraded Short-RangeMissile Was a Success
TEHRAN (AP) - Iran said Saturday that it had
successfully test-fired an upgraded version
of a short-range ballistic missile with
improved accuracy, increasing its capacity
to strike land and naval targets.
Iran's defense minister, Brig. Gen. Ahmad
Vahidi, said the solid-fueled Fateh-110
missile had a range of 185 miles. He also said
the weapon could strike with pinpoint
precision, making it the most accurate
weapon of its kind in Iran's arsenal.
"By reaching this generation of the
Fateh-110, a new capability has been added
to our armed forces in striking sea and land
targets," state television quoted General
Vahidi as saying. Iran's military leaders have
said they believe that future wars will be air-
and sea-based, and Tehran has sought to
upgrade its air defense systems and naval
power in anticipation of such a possibility.
TETESI: MEMBE AKALIA 200BN/= ZA ZANZIBAR
Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya nchi
za Nje na “Ushirikiano wa Kimataifa”
amekalia pesa za Zanzibar zipatazo 200bn/=
zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuipa
Zanzibar kuendeleza/kufufua specifically
zile EPZ, maeneo huru ya kiuchumi Zanzibar.
Waliotoa pesa hizi wakiwemo UAE/Rasil
Khemah – ambao viongozi wetu wote
watatu (Shein, Seif-1 na Seif-2) wamekuwa
kiguu na njia kutafuta misaada. Imepatikana
Membe – laatul laah amezuia, just kutia saini
tu ili pesa ziwe released.
Kipengelea kimoja kinachomfanya Membe
ndiye atiwe saini/pesa za misaada, mikopo,
zawadi n.k zinapoingia katika foreign
currency au misaada kama hiyo – Zanzibar
hairuhusiwi kusaini, kwa sababu ‘si nchi’
inatakaiwa TZ ndio imwage wino.
Huu ni mwezi wa pili, Membe amekalia
barua yetu na pesa zetu, halali yetu.
Baadaye wanakuja Zanzibar eti kujiliza
baada ya meli kuzama.
Hiyo ndio TZ, na huo ndio Muungano wetu
uliodumu miaka 48 kwa Bara kuidhulumu
Zanzibar.
* Plus, jana tu Abubakar alikuwa anasema
ndani ya BLW kuwa hao hao akina Membe
wameinyima Zanzibar fursa ya kuhudhuria
vikao muhimu vya kimataifa kwa
kuwanyima wajumbe wake visa, just kwa
sababu wao watanganyika hawakwenda au
hawakutakiwa kuwemo.
Ushauri wangu: MAMBO YA NCHI Z ANJE
IONDOSHWE KABISA KATIKA LIST YA
MUUNGANO (GET ME RIGHT PLEASE, SIO SUALA
LA KUGAWANA MABALOZI, LA HASHA). ONDOA
FOREIGN AFFAIRS KATIKA LIST HIYO FOR
GOOD.
Mbaya zaiid katika sakata hili la Membe
kuzuia pesa zetu, naibu wake anaitwa
Mahadhi Juma Maalim – mzanzibari wa
Muyuni/na Mungoni (huyu ni kambi ya NO
vote katika referendum, na ndiye group la
akina Samia, Haroun, Shamsi, Perera Ame
Silima – wanachochea watu wa kusini
wasema NO serikali tatu au muungano wa
mkataba). Mahadhi, Kazi ya uzinzi haifai na
kutafuta wanawake kuowa. Kuwa na akili
wewe, nchi yako inazamishwa.
Hizi habari za Membe kukalia 200bn/=
zimeigusa BLW na cabinet ya Zanzibar – ni
habari zilizoleta ghazab sana, maana hili si la
mwaka 1968 au 1980s au 1970s – it’s only
two months ago or less (jana na leo).
Source mzalendo.net
WAUMINI WA KIISLAMU VISIWANIZANZIBAR WAAMUA KUMUACHIA M/MUNGU ATOE HUKUMU KWA WALEWOTE AMBAO HAWAITAKII MEMAZANZIBAR
Maelfu ya waislamu nchini zanzibar
wameamua kujikusanya katika msikiti Afraa
ulioko kidongo chekundu kwa ajili ya
kumshtakia M/mungu juu ya suala zima la
kukashiwa na kufanyiwa vitendo vya
uonevu na wale ambao hawaitaki mema
nchi ya zanzibar.
Mkusanyiko huo ulikua na lengo la kuomba
Dua maalum ambayo imeeandaliwa na
jumuiya ya muamsho zanzibar kwa lengo la
kuwaunganisha waislamu ili wawe kitu
kimoja katika kudai na kutetea maslahi ya
nchi yao,vile kumuomba mungu awanusuru
viongozi wa harakati za kuitakia mema
zanzibar na shari za maadui zao, katika dua
hiyo kuliambatana na uchinjaji wa
wanyama tofati kwa ajili ya sadaka ambayo
walipewa mayatima na wanawake.
Akibainisha idadi ya vichinjwa hivo amir wa
jumuiya hiyo SH FARID HADI amesema jumla
ya ngombe saba, mbuzi 33, kondoo 3, kuku
22, bata 1 na njiwa 1 wamekabidhiwa na
wamewachinja wote.
Kwa upande wao viongozi wa jumuiya ya
muamsho wameweza kujichinjia wanyama
kwa mikono yao kwa kushirikiana na
waumini wengine ambao walibahatika
kuwepo katika viwanja vya uchinjaji.
Amesema dua hii imeamuliwa kuwekwa
mwezi 17 Ramadhan kwasababu tarehe hii
ina historia kubwa katika ushindi wa
waislamu. kwani siku kama hii ndio siku
ambayo Allah aliwanusuru waislamu katika
vita vya badri.
Aliongeza kwa kusema waisalmu
wanatakiwa wawe na umoja wa ukweli
ukweli ili kuweza kuwashinda maadui zao
na kupata ushindi kwa yale wanayoyahitaji.
Nae kwa upande wake sh MSELEM bin ALLY
AMEWAOMBA waislamu waendelee na
msimamo wao ule ule wa kutokushiriki
suala zima la sensa ambayo inategemewa
kufanyika hvi karibuni.
Source mzalendo.net
Wednesday, August 1, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)