Wednesday, August 8, 2012
Marekani yataka Rwanda kusitisha Msaada kwa Waasi wa M23
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
Hillary Clinton ameitaka serikali ya
Rwanda kuisaidia Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo DRC
kuwanyang'anya silaha waasi wa M23
na kusitisha msaada kwa Kundi hilo kwa
lengo la kupata suluhu ya mgogoro wa
Mashariki mwa nchi hiyo.
Clinton amesema wanataka kuona nchi za
Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR zinashiriki
kikamilifu katika kurejesha usalama nchini
DRC na kulisambaratisha Kundi la Waasi la
M23 ambalo linatekeleza mashambulizi
Mashariki mwa nchi hiyo.
Kauli hii inakuja kipindi hiki ambacho
Viongozi kutoka nchi kumi na moja za
Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiwa
kwenye mkutano wa siku mbili nchini
Uganda kujadili usalama wa DRC ili
kulimaliza Kundi la M23.
Clinton ametaka Viongozi hao wa Ukanda
wa Maziwa Makuu kutathimini kwa kina
namna ya kuweza kushughulikia mgogoro
huo na hatimaye kurejesha utulivu ambao
umepotea Mashariki mwa DRC.
Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa
Makuu ICGLR umeingia siku ya pili ambapo
Rais wa DRC Joseph Kabila Kabange
hatukutana tena na Rais wa Rwanda Paul
Kagame kama ambavyo ilipangwa awali na
badala yake wataandaliwa kikao chao
pekee.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Oriem
Okello amesema Viongozi hao wawili
hatokutana na badala yake Rais Yoweri
Kaguta Museveni ataandaa mkutano baina
yao na kwa sasa wamejiegemeza kujadili
kupata Jeshi litakalolinda amani mpaka mwa
DRC.
Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu ICGLR
wataamua Kikosi ambacho kitaenda kulinda
mipaka ya DRC na kukabiliana na uasi
ambao unafanywa na Kundi la Waasi la M23
ili kusaidia juhudi za amani.
DRC yenyewe imeshaainisha haitaki nchi ya
Rwanda ishirikishwe kwenye Jeshi hilo
kutokana na kudaiwa kuwafadhili Waasi wa
M23 huku Kigali yenyewe ikishinikiza
inataka kushiriki kwenye mpango wa
kurejesga amani.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Shirika la
Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa
OCHA Valerie Amos anaendelea na ziara yake
kuangalia madhara ya mashambulizi ya
Kundi la M23 nchini DRC.
Amos amesema hali ni mbaya Jimboni Kivu
kitu ambacho kama hakijadhibitiwa
kinaweza kuzua maafa zaidi kwa wananchi
wa eneo hilo kutokana na mashambulizi ya
mara kwa mara ambayo yamekuwa
yakifanywa na Kundi la Waasi la M23.
Kundi la Waasi la M23 limeendelea
kujigamba kupiga hatua kwenye
mapambano yake na Jeshi la Serikali hasa
katika maeneo ya Rutchuru na sasa
wanaendelea kusaka uungwaji mkono
kutoka kwa wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment