Sunday, August 12, 2012
Wakenya 13 wafariki dunia katika ajali ya mabasi ilotokea tanzania
Idadi ya watu walofariki katika ajali ya
mabasi mawili karibu na mji wa Tanga
Tanzania Ijuma asubuhi imefikia 13. Watu
42 wamejeruhiwa miongoni mwao 14
wako katika hali tabani, watu 29
hawakujeruhiwa.
Walofariki ni miongoni mwa kundi la
wanawake wa Kenya kutoka kanisa la
Presbyterian Church of East Africa - PCEA
kutoka Thika walokuwa wanasafiri kuelekea
Dar es Salaam kwa sherehe za kidini
Tanzania.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani
Tanzania, Ernest Mangu ameiambia sauti ya
Amerika kwamba serikali ya Kenya
inashirikiana kwa karibu sana na Tanzania
na imepeleka ndege maalum kuwasafirisha
nyumbani walonusurika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment