Sunday, August 12, 2012
Waislamu wa Myanmar wazidikuteseka
Ripoti mbalimbali kutoka Myanmar
zinasema kuwa maafa makubwa yanatokea
katika kambi ya wakimbizi wa Kiislamu
katika jimbo la Rakhine. Kanali ya televisheni
ya Press imeripoti kuwa watu karibu 20
wakiwemo watoto wadogo wamefariki
dunia katika kambi hiyo ya Waislamu wa
jamii ya Rohingya huko Myanmar kutokana
na ukosefu wa dawa na chakula. Ripoti hiyo
inasema vijiji kadhaa vya Waislamu wa
kaskazini magharibi mwa Myanmar
vimeteketezwa kwa moto na Mabudha
wanaosaidiwa na jeshi la polisi, na wakazi
wa vijiji hivyo wamelazimika kuwa
wakimbizi. Mabudha hao wenye misimamo
mikali pia wamechoma moto misikiti
kadhaa. Umoja wa Mataifa umesema kuwa
ukatili wanaofanyiwa Waislamu wa
Myanmar ndiyo mkubwa zaidi kuwahi
kushuhudiwa duniani katika siku za hivi
karibuni. Shirika la Kutetea Haki za
Binadamu la Human Rights Watch (HRW)
limesema kuwa jeshi la Myanmar limetenda
jinai nyingi dhidi ya Waislamu wa Rohingya
walio wachache. Ripoti hiyo imefafanua
kuwa miongoni mwa jinai hizo ni kubakwa
wanawake wa jamii hiyo ya Waislamu
kaskazini mwa Myanmar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment