Sunday, August 12, 2012
MISRI YATUMA VIKOSI VYAKE SINAI
Misri imetumia Helicopter kufanya
mashambulizi ya mizinga dhidi ya
wakereketwa wenye imani kali walio
katika eneo la Sinai tangu mwaka
1973 katika kile jeshi la Misri
lililochotaja kama shambulio la
kurejesha utulivu.
Matumizi ya anga ni ishara ya
mabadiliko ya vita vya Misri dhidi ya
wakereketwa wa Kiislam ambao
wamezidisha shughuli zao katika
eneo lenye milima na jangwa lenye
mpaka na Israili na Gaza.
Mapema wiki hii wapiganaji
wakereketwa waliishangaza Misri
kwa ujasiri wao kwa shambulizi
ambamo askari 16 waliuawa, magari
ya jeshi yakaibwa na kuelekea Israel
kwa lengo la kujaribu kufanya
shambulio jingine.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye
televisheni ya taifa jeshi limesema
kua limeanzisha operesheni ya
mchanganyiko wa vikosi kwa kutaka
kurejesha utulivu huko Sinai, majeshi
yakiungwa mkono na Jeshi la anga.
Shambulio la siku ya jumapili ndio
baya kuwahi kufanywa huko Sinai
kwa miaka mingi na hatari kuliko
yote dhidi ya vikosi vya Misri
ikiashiria ongezeko la vitendo
vinavyokiukaq sheria katika eneo
hilo.
Katika tukio la hivi karibuni, watu
wenye silaha waliwafyatulia risasi
walinzi kwenye vizuizi huko El -arish,
mji mkuu wa Wilaya ya Sinai, mji ulio
umballi wa kilomota 50 kutoka
mpaka wa Gaza na Israili.
Ghasia kwenye mpaka wa Israel na
Misri inaweza kutishia mkataba wa
amani baina ya nchi hizi mbili.
Hio ndio sababu Israel imeiambia
Misri ichukue hatua za kusuluhisha
vurugu badala yake kupeleka vikosi
vyake. Israel imekubali kuondoa
baadhi ya masharti yanayozuwia
shughuli za kijeshi katika Sinai ili Wa
Misri waweze kuingiza vikosi zaidi.
Lakini uvamizi wa Misri dhidi ya kile
walichokiita magaidi hautobadili
lolote katika sehemu ya Sinai
inayokaliwa na makabilia ya Wa
Bedwini wenye fikra huria.
Ni eneo linalovutia kwa makundi
ambayo yangependa kutumia
sehemu isiyokua na utaratibu
wowote wa uongozi kwa aijili ya
kuifika Israili.Rais wa Misri
Mohammad Mursi aliahidi kwamba
atadhibiti eneo la Sinai kwa
ukamilifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment