Tuesday, August 7, 2012
MALAWI Vs TANGANYIKA( TANZANIA BARA )
Malawi imekataa kuitikia wito wa
Tanzania kutaka isimamishe shughuli
za kutafuta mafuta na gesi ziwa
Malawi, wakati suluhu ya mvutano
wa mpaka ikisubiriwa.
Mvutano wa maneno umezuka kati
ya nchi hizo mbili baada ya Malawi
kuipa leseni Kampuni ya Uingereza
kufanya utafiti katika eneo hilo.
Maafisa nchini Tanzania wanasema
mvutano huo uliodumu kwa miaka
50 sasa unaweza kuwa mkubwa
iwapo ugunduzi wa mafuta na gesi
utatokea kwenye ziwa hilo
linalojulikana kama Ziwa Nyasa
nchini Tanzania.
Tanzania inasema inaendelea
kufanya mazungumzo na Malawi na
iko Tayari kulipeleka suala hilo
kwenye vyombo vya upatanishi.
"Hili ni suala nyeti sana na
tungependa litatuliwe kwa
maelewano, tutaendelea na
mazungumzo," Waziri wa Mambo ya
Nje wa Tanzania alisema.
Membe wiki iliyopita alviambia
vyombo vya habari nchini humo
kuwa "shughuli za uchimbaji katika
eneo la kaskazini mashariki mwa
ziwa hazina budi kusitishwa kupisha
mazungumzo kutatua mzozo huo
yafanyike."
Malawi, koloni la zamani la Uingereza,
kwa upande wake iliapa kuendelea
na chughuli za utafiti wa hewa gesi
mkaa (hydrocarbons).
Tanzania,lililotawaliwa na Ujerumani
na baadaye Uingereza, inadai kuwa
sehemu ya kilometa za mraba
29,600 sawa na maili 11,400 za ziwa,
wakati Malawi inarejea makubaliano
ya mwaka 1890 yanaonyesha kuwa
mpaka kati ya nchi hizo mbili uko
kwenye ufukwe upande wa
Tanzania.
Msumbiji pia inadai ina sehemu yake
katika ziwa hilo la tatu kwa ukubwa
barani Afrika.Mwezi Septemba
mwaka jana serikali ya marehemu
Bingu wa iliipa leseni kampuni ya
Surestream Petroleum, kutafiti
mafuta na gesi ziwani.
Mataifa hayo mawili yatafanya
mazungumzo juu ya mpaka
kaskazini mwa Malawi katika mji wa
Mzuzu Agosti 20 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment