Friday, August 7, 2015

JUSA: TUNAHESHIMU MAAMUZ YA LIPUMBA

Chama cha wananchi CUF kimetoa kauli juu ya kujiuzulu kwa alie kua mwenyekiti wa CUF taifa prof Ibrahim haruna Lipumba.
Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkurugenzi wa habari,uenezi,na mawasiliano na Umma Mhe Ismail jussa ladhu,Imesema kwamba CUF imepokea taarifa hiyo na inaheshimu maamuzi yake pamoja na kuwahiidi wanachama kua CUF haitayumba
"Tunapenda kuwahakikishia wanachama na wapenzi wa CUF na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwamba chama hichi hakitayumba"
alisema Ismail jussa
Mhe ismail jussa amesema CUF itaendelea kumheshimu kwa utumishi wake mkumbwa ndani ya chama pamoja na kuthamini mchango wake katika ujenzi wa demkrasia katika nchi yetu.
Kuondoka kwa proffessa lipumba katika Safu ya uongozi wa Cuf kutaacha pengo kubwa hasa kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Proff lipumba ni miongoni mwa waazilishi wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ambao utamsimamisha waziri mkuu wa zamani Mhe Edward lowassa kama mgombea wake.

No comments:

Post a Comment