Thursday, August 6, 2015

Ukawa, Ccm zagawanyika

Wakati sintofahamu ya nini hatma ya dk wilbroad slaa bado haijafahamika ndani ya chadema,leo umoja wa katiba ya wananchi wamepata pigo jingine baada ya Mmoja kati ya nguzo muhimu ya ukawa kujiengua. Profesor Ibrahim lipumba ambaye alikuwa mwenyekiti wa CUF kwa takriban miaka 10 na zaidi ameamua kujiondoa katika nafasi hiyo katika chama chake na kusema kuwa atabaki kuwa mwanachama wa kawaida kwasababu kadi yake ya chama inakwisha muda wake mwaka 2020. Akiongea na waandishi mjini Dar es salaam profesa amesema kuwa amejiondoa nafas yake kwasababu ya cjadema kukiuka misingi ya makubaliano yao na hapendi kuwa miongoni mwa watu watakaoshiriki dhambi ya kuwadhulumu watanzania. Jaya yanatokea siku kadhaa baada ya chadema kumtangaza Edward lowasa kuwa mgombea wake na wa ukawa.

No comments:

Post a Comment