Thursday, June 28, 2012

pinda akwepa kujiuzulu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema hawezi kujiuzulu kwa madai kuwa ameshindwa kutatua matatizo ya madaktari. Pinda amelieleza Bunge kuwa, hadhani kama ni busara kujiuzulu kwa sababu ya matatizo ya madaktari na kwamba suala hilo ni la muda mrefu na ni changamoto. Waziri Mkuu ametoa msimamo huo wakati anajibu swali la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ambaye alisema, kwa kuwa matatizo ya madaktari ni ya muda mrefu, na Pinda ameshindwa kuyamaliza, kwa nini asijiuzulu. Waziri Mkuu amelieleza Bunge kuwa, amefanya kila aliloweza kumaliza mgogoro kati ya Serikali na madaktari. Lissu alimuuliza Pinda kuwa, kama amefanya kila aliloweza kumaliza tatizo hilo na ameshindwa kwa nini asijiuzulu. Waziri Mkuu amemjibu kwamba, anamuheshimu sana, na hadhani kama hiyo ni namna nzuri ya kumuuliza. Spika wa Bunge, Anne Makinda, amefunga mjadala kuhusu mgogoro wa Serikali na madaktari kwa kuwa Mahakama imelalamika kwa kuwa, suala hilo lipo mahakamani lakini wabunge wameendelea kuuliza, kudadisi na kutoa taarifa. Kutokana na msimamo huo wa Bunge, Serikali leo haitatoa msimamo wake kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea katika hospitali nyijngi nchini zikiwemo hospitali za rufaa. Makinda ametoa msimamo huo wakati anatoa mwongozo alioomba Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye alimuomba aagize Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii itoe taarifa bungeni kuhusu waliyoyaona walipotembelea hospitali na kuzungumza Serikali, madaktari, na wadau wakati wa mgomo uliopita wa madaktari. Makinda amewaeleza wabunge kuwa, yeye ndiye aliyeituma kamati kufanya kazi hiyo, na ilitoa taarifa kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uongozi hivyo taarifa hiyo haitawasilishwa bungeni. “Sasa suala hili lipo mahakamani na huo mjadala umefungwa”amesema Makinda.

Silencing the Trolls: Twitterconsiders ‘hate speech’censorship

Is Twitter allowing too much freedom? What helped move revolutions along in the Middle East, has a flip side of cyberbullying and abuse, especially of those in the spotlight. Now Twitter is taking its first step towards censorship. The news was broken by Twitter’s Dick Costolo who was speaking to the Financial Times. As the FT put it, the site’s chief executive “became visibly emotional” as he described his frustration in tackling the problem of ‘horrifying’ abuse, while maintaining the company’s mantra that ‘tweets must flow’. Anonymous and unpunished, irresponsible twitter-users find the site ideal for expressing all kinds of extremist, racist and sexistopinions. Celebrities are among those most vulnerable, with curses and bullying clogging up their ‘@connect’ section, offending many and disrupting conversations, often turning them into hate-fights. To stop the ‘hate speech’ anarchy, Twitter is considering starting off by blocking the very possibility of replies from so-called ‘non- authoritative’ users, marked out by the absence of a profile picture, followers or bio information, as FT.com reports. This is the first step, but there might be more to come. However, the company’s management is concerned that by installing any kinds of ‘selective’ measures, they may put an end to the unique Twitter-style ‘freedom of tweets’ that has helped Arab revolutions. Anonymity was the key factor that allowed so many users there to join and have their say. “The reason we want to allow pseudonyms is there are lots of places in the world where it's the only way you'd be able to speak freely," FT quotes Dick Costolo as saying. Twitter is basically the ‘last harbor’ of anonymity, as it does not have to be linked with such powerful database platforms as Facebook and Google. Silencing trolls may hit those ‘revolutionary’ users as well. The reality is that Twitter’s move may be coming at the right time, as websites that allow comments and replies may soon be forced to identify online bullies, or ‘trolls’, under different legislative moves. In the UK, for example, the Defamation Bill is now passing through the House of Commons, which will allow direct legal action against online offenders. Justified or not, ‘troll’ censorship will surely open a new page in Twitter history.

Dr.Shein kutetea muungano kinyume namatakwa ya wananchi ?

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema ataendelea kuutetea Muungano na hakuna atakaemlaghai wala kumchezea katika uongozi wake. Kauli hiyo ameitowa jana katika mkutano wa Jumuiya ya Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Bwawani mjini Unguja. Dk Shein amesema kwamba yeye ndie rais wa Zanzibar na ndie mwenye mamlaka na hatomuogopa mtu wala kusita kuwachukulia hatua kwa wale wote ambao watakwenda kinyume na matakwa ya kikatiba. Alisema kuwa dhamana ya nchi hii pamoja na ile ya Jamhuri ya Muungano imo mikononi mwao kati yake na Rais Jakaya Kikwete na ndio maana wakawa wanashirikiana na kushauriana kwa yale yote ambayo yana maslahi na nchi. “katika kuiongoza Zanzibar mimi ndie rais simuogopi mtu yeyote”, alisema kwa kujiamini Dk Shein. Dk Shein alisema Zanzibar ni nchi ya kidemokrasia inayotoa uhuru wa maoni kwa kila mtu, lakini kwa upande wake pia yeyé ndio mwenye dhamana kubwa ya kuendesha nchi kwa mujibu wa katiba iliyopo. “Mimi ndio rais siogopi mtu katika kuendesha nchi, siko tayari kuirudisha nchi katika misukosuko na kuirejesha Zanzibar kule ilipotoka wakati iko katika hali ya amani hivi sasa,” alisema katika mkutano huo. Hata hivyo alisema kuwa Muungano upo na utaendelea kuwepo na kwani yeye ndiye rais ambaye anatokana na chama cha mapinduzi na pia ameingia madarakani chini ya ilani ya chama chake hivyo lazima afuate ilani ya chama chake ambapo alisema changamoto zilizomo zinahitaji kujadiliwa ili kuweza kuziondoa na sio kuvunja muungano. “Hakuna mtu asiyejua kuwa kuna kero za Muungano hivyo ni vizuri tukajitokeza kwa wingi katika kutoa maoni yetu juu ya katiba na sio kukaa pembeni yanazungumzwa mengi kuhusu mimi lakini yote nimeyapokea kwa kuwa ukubwa ni jaa”, alisema Dk Shein bila ya kutaja jina lakini alikuwa akijibu hoja zilizokuwa zimeibuka kuwa hana uwezo wa kuchukua maamuzi magumu katika suala la uongozi. Aliwaeleza wastaafu hao kwamba Muungano una kero, zinazojadiliwa na ndio maana njia nyingi, ikiwemo ya mawasiliano baina ya Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeanzishwa ili kuzitafutia ufumbuzi ambapo alisema njia hizo zitaendelea kutatua mambo ya muungano. Aidha Dk Shein alisema kazi hiyo anaifanya kwa umakini ili kuhakikisha kuwa Muungano upo na unazidi kuwepo na kwamba wasioutaka wasubiri tume ikija ndio watoe maoni yao na sio kuanza kutoa maoni hivi sasa kabla ya wakati hufika. “Hakuna asiyejua katika Muungano kuna kero,… wananchi wazijadili kupitia tume ya mabadiliko ya katiba, na kwa nini tunaanza kusema sema… subirini tume mkatoe maoni yenu” alisema. Katika hatua nyengine Dk Shein alisema kwa sababu hiyo anaagiza kutokufanyika kwa maandamano ya aina yoyote kuhusiana na suala hilo na kuwataka wazanzibari kutoshiriki hadi pale wanaotaka kufanya hivyo wanaporuhusiwa kuandamana na jeshi la polisi kwa kufuata taratibu za kisheria. “Naagiza maandamano yasifanyike,… wakiruhusiwa kufanya basi msiende kushiriki,” alisisitiza Dk Dk Shein alikuwa akizungumza na zaidi ya watu 500, waliohudhuria katika mkutano huo, ambao ni wastaafu wa taasisi za Muungano waliopo Zanzibar. Katika waliohudhuria katika mkutano huo ni taasisi mbali mbali pamoja na Bunge, Ulinzi na Uslama, Mambo ya Nje, Mamlaka ya hali ya hewa (TMA), Mamlaka ya Kodi na mapato (TRA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Idara ya Uhamiaji, Shirika la Posta na Simu, na taasisi za masuala ya elimu na ufundi. Sambamba na hayo aliwataka vijana kuthami ni jitihada, michango na maelekezo ya wastaafu kwa kutambua kuwa uzoefu wao katika maisha ni sehemu muhimu kwa maendeleo yao. “Sote hatuna budi kuelewa kuwa iko siku tutakuwa wastaafu hivyo ni muhimu kujitayarisha hasa kwa kujenga tabia ya kujiwekea akiba na matayarisho mengine ya lazima kwa maisha ya wastaafu”, alisema. Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo , Mohamed Ali Maalim, alisema miongoni mwa majukumu ya jumuiya hiyo ni kudumisha Muungano kwa sababhu unalinda maslahi ya wastaafu wote nchini. Katika risala yao wastaafu hao wamesema kwamba wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ndani ya Jumuiya yao ikiwemo uwezo mdogo wa uendeshaji na usimamizi wa ofisi ikiwemo ukosefu wa ofisi ya kutosheleza mahitaji. Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Rashid Ali alitaja changamoto nyengine ni kukosekana kwa wataalamu na waratibu wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya Jumuiya, ukosefu wa vitendea kazi, ukkatika kutekeleza malengo yao. Jumuiya ya wastaafu Zanzibar imeanzishwa mwaka 2009 ina wanachama 537 ambapo 486 kati ya hao ni wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Source mzalendo.net

Ni ipi siri ya Muungano,Watanganyikawanaogopa nini ?

Leo ni takriban miaka 48 ya Muungano kati ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Tanganyika tokea kuasisiwa kwake baada ya Mapinduzi,lakini kwa walio wengi hususani Wazanzibar wameshindwa hasa kujua ni ipi hasa siri ya Muungano huu.Kumekuwa na madai mengi na fikra tofauti kuhusu Muungano huu kutoka kwa watu na taasisi mbali mbali ndani na nje ya nchi. Ni dhahiri kwamba mwisho wa yote Muungano huu utamalizika au utaendelea mbele ukiwa na uhasama mkubwa kuliko udugu,upendo,maelewano na maendeleo kama wanavyodai wale wote wenye hoja ambazo wanautetea Muungano huu wenye hila na siri nzito, hususani Viongozi wa Serikali walioko madarakani wale wa Bara na baadhi ya wale Wahafidhina wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ambao hutumiwa kama chambo zidi ya Wazanzibar wenzao. Katika Muungano huu tokea siku ya mwanzo , kumekuwa na tuhuma nyingi kiasi ambacho kwa mwenye akili timamu hatosita kuelewa kwamba ndani yake kuna siri nzito zidi ya Taifa moja. Kwa walio wengi wanakumbuka kwamba unapolitaja neno Muungano hapo zamani ilikuwa ni kosa la jinai na adhabu yake kwa wakati huo ilikuwa kifo.Wako Wazanzibar wengi ambao walikuwa Wasomi,wanafalsafa,wanasiasa,madokta pamoja na Wananchi wa kawaida walipoteza maisha yao kwa kupinga au kuhoji Muungano huu,lakini kama haya hayatoshi hadi hii leo bado Wazanzibar wanaonekana kama ni maadui pale tu wanapoligusia suala zima la kudai haki yao ndani ya Muungano. Tuangalie kama vile jumuia ya Uamsho ambayo imejitolea kwa ridhaa yao kuwaelimisha Wananchi juu ya haki zao za msingi kudai Nchi yao huku wakifuata sheria za Nchi,hapa pana kuna kosa gani kwa Mwananchi kujielewa na kujua haki zake za msingi? Nilifikiria ya kwamba Serikali zote mbili zitawapongeza kwa vile Jumuiya hiyo imejitolea kihali na mali kutoa elimu kwa Wazanzibar, jambo ambalo Serikali zote mbili zimeshindwa kulifanya kwa Wananchi wake. Kichekesho ni kuona Muungano huu wa Nchi mbili huru, mara zote wanaolalamika kuonewa ni upande mmoja wa Muunganoyaani Zanzibar, lakini zaidi wanaopiga kelele kwa kuumia ni wananchi wanyonge walio wengi na si Viongozi wa Serikali zote mbili.Pia la ajabu ni kwamba Watanganyika wamerizika na wala Wananchi wake hawana madai kwamba wanaonewa na zaidi wanapendelea Muungano huu uzidi kuimarika. Hapa tutapata picha halisi kwamba ni dhahiri Watanganyika wanafaidika sana na hali hii iliopo hivi sasa.Isitoshe Watanganyika mara zote hutoa vitisho kwamba pindipo Muungano ukivunjika basi Zanzibar na hasa Wapemba ndio watakaoumia kwa vile wamejiimarisha sana huko wamejenga magorofa, hii inaonesha kwamba kuna lengo la kuwafukuza Wazanzibar Tanganyika kama kuwapa adhabu, watu wanasahau historia kwani Zanzibar baada ya Mapinduzi baadhi ya watu walinyang’anywa majumba yao, mashamba na vyenginevyo na hadi sasa watu wanaishi. Sasa huo udugu unaozungumziwa na Watanganyika ndio huo ? Jee wale Wazanzibar au Watanganyika wanaoishi United kingdom,Canada,Marekani,Falme za kiarabu nao pia warejeshwe maanake hawa wote hawakuungana na Nchi hizo, nako huko pia wamejiimarisha hizo ni propaganda za kijinga na ulimbukeni. Nashindwa kuelewa kuona Watu ambao wanajiita Wasomi wa Watanzania wakiwemo , Marais,Mawaziri,Wabunge,Wawakilishi na Waandishi wa habari wanashindwa kufahamu maana ya Nchi kuwa huru,haki za binaadamu,uhuru wa kuabudu,demokrasia ya kweli,usawa kwa wote, lakini pia dhana ya Muuungano kwa Nchi husika ni nini. Naamini wangalifahamu dhana hizi basi wangeliondokana na zile kasumba na fikra za ukandamizaji zilizoletwa na Wakoloni weupe na baadae kurithishwa kwa Wakoloni weusi kama vile Mwalimu Nyerere na baadhi ya Viongozi wa Afrika ambao kwao wao mabadiliko ya kidemokrasia ni mwiko. Sisi kama kizazi kipya tunaenda kwa misingi ya mabadiliko ya ulimwengu na teknolojia,sasa yale mawazo ya vijiji vya ujamaa watu kuishi maporini na Azimio la Arusha yamepitiwa na wakati lazima Serikali walielewe hilo. Nimekuwa nikishangaa sana kuona Serikali ya Tanganyika inajaribu kufanya kila inavyowezekana kujaribu kuzuia na kuzima wimbi la Wazanzibar kupasua bahari na kuelekea Nchi kavu,kuna haja ya kujiuliza kulikoni ? Jee hii ni haki kwa nchi mbili zenye haki sawa na zilizoungana kwa hiari ?Mbona inaonekana zaidi kwamba Taifa moja linalitawala jengine. Muungano huu umekuwa ni ndoana kwa Wazanzibar na tusifikirie kwamba ndoana hii kwa vile tumeshaimeza tutakuwa salama hata tukiitoa basi lazima tushikamane. Watanzania lazima tukubali kwamba mabadiliko katika Muungano huu ni jambo la lazima kama kufa na mwanaadamu,tukidharau basi tukubali kwamba madhara yake yatakuwa makubwa kuliko faida yake. Wazanzibar wamechoka na utashi wa watu binafsi kujiona kwamba Zanzibar ni miliki ya kikundi fulani,watu fulani, chama fulani,fikra kama hizo zitatufikisha pabaya. Leo hii imekuwa ni mazoea kwa Serikali ya Tanganyika kuwanyanyasa Wazanzibar kwa kutumia vitimba kwiri na Wahafidhina wa Kizanzibar waliopandikizwa kuzima madai ya Wazanzibar kuhoji uhalali wa Muungano.Imekuwa kama desturi kwa Viongozi wa bara hasa wastaafu akina, Ali Hassan Mwinyi,Benjamini mkapa kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar lakini pia kuzidisha hasama miongoni mwa Wazanzibar, hali hii tutaenda nayo mpaka lini.Sio kweli kwamba wanawapenda Wazanzibar bali wanayafanya hayo kulinda maslahi yao binafsi.Wakati umefika kuachiwa Wazanzibar wajiamulie mambo yao wenyewe, na kuwa Taifa huru,hivi Watanganyika wanaogopa nini ? Muungano huu umekuwa kama ni chaka ambalo limeficha siri nzito,linalindwa kwa nguvu zote za dola lakini kubwa zaidi ni kuona hata waandishi wa habari kule bara wanashirikiana vizuri na Serikali yao ili kuisadia kuwakandamiza Wazanzibar kudai haki yao. Nimekuwepo Zanzibar kwa muda mrefu sasa, nimeona na kushuhudia mengi yanayotokea hapa Zanzibar lakini takribani waandishi wote wa habari wanashirikiana na vyombo vya dola kuficha ukweli na kuzidi kuwaona Wazanzibar kama vile ni maadui pale wanapodai haki yao ya msingi ndani ya Muungano.Nilifikiria kuona kama vyombo vya habari vitakuwa mstari wa mbele kufichua uovu katika jamii yetu kinyume chake ndio wao wanaoikandamiza Jamii yetu kwa fitna,uongo na ubabaishaji wa habari na matukio ya kweli.Fahari ya vyombo vya habari pamoja na waandishi waTanzania ni kutangaza propaganda za Serikali na jinsi ya kuwadhibiti Wananchi ili waone kwamba umaskini tulionao ndio maumbile yetu ,sasa hio demokrasi inayozungumziwa na katiba mpya inayotegemewa ipo wapi. Ukweli unafichwa na propaganda ndizo nyimbo za Waandishi wa habari na baadhi yao tayari wanafanya kazi ya serikali ya Tanganyika kupotosha wananchi na ulimwengu kwa jumla ukweli na uhalisia wake.Sasa taaluma hii ya uandishi ina maana gani kwa Watanzania,ikiwa yale maovu yaliotawala kwenye jamii yanashindwa kufichuliwa.Hii ni kutokana na serikali ya Tanganyika kuwarubuni kwa nia ya kuendeleza sera ambazo kwa ulimwengu huu tunaokwenda nao hazikubaliki tena. Ingawaje Serikali ya Tanganyika imejipanga vizuri kwa kupenyeza vibaraka wake ndani ya Zanzibar ambao huwalai kwa madaraka baadhi ya Viongozi ili iwe rahisi kwao kuwathibiti Wazanzibar ni vyema baadhi viongozi hawa wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakaelewa kwamba hivi sasa maji yameshamwagika,Wazanzibar wameshikamana kudai haki yao na hapana budi kuungana nao ili malengo ya Wazanzibar yafanikiwe kwa usalama na amani bila ya kumwaga damu.Ule wakati wa kugombea vyeo umeshapitiwa na wakati,huu nu wakati wakuona Kwamba Jamhuri ya watu Wazanzibar kwanza,baadae ndio tuangalie utawala na mstakabali wetu kwa pamoja. ZANZIBA KWANZA: source mzalendo.net

Tuesday, June 26, 2012

Mbunge ataka vigogo wauziwemashangingi

MBUNGE wa Viti Maalum, Martha Mlata (CCM) amesema, magari ya Serikali yanatumiwa vibaya hivyo yauzwe kwa watumishi wa umma ili kupunguza matumizi yasiyo na tija. Mbunge huyo amesema, Serikali itumie waraka uliotolewa wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili kuyauza magari hayo kwa watumishi, na kwamba, kila anayestahili apewe gari kulingana na kazi anazofanya na wadhifa wake. “Nilikuwa najiuliza, waraka ule ulifutwa au umepitwa na wakati? “ ameuliza Mbunge huyo bungeni mjini Dodoma wakati anachangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, licha ya Serikali kutoa waraka huo, magari ya Serikali yalitumika kufanya kazi binafsi za watumishi wa umma, na zikaandaliwa bajeti za kununua magari mengine ya Serikali. Mlata amesema, itakuwa busara kama Serikali itayauza magari hayo kupunguza matumizi ya Serikali na amedai kuwa Tanzania ni nchi pekee Afrika Mashariki inayotumia magari isivyostahili. Mbunge huyo ameliembia Bunge kuwa, huwa anasikia aibu wakati wa sherehe za kitaifa, kwa kuwa mabalozi wa nchi wahisani huwa wanakwenda uwanjani wakiwa kwenye gari la pamoja lakini viongozi Watanzania huwa wanashindana kwa magari. Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema) amesema, uamuzi wa Serikali, kuweka ukomo wa ukubwa wa injini za magari yanayoweza kununuliwa na Serikali Kuu, taasisi zake na mamlaka za Serikali za Mitaa hautakuwa na tija kama magari ya kifahari yaliyopo sasa hayatauzwa. “Haya yangeuzwa halafu tukanunua mengine” amesema Nyerere bungeni mjini Dodoma wakati anachangia bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametangaza bungeni uamuzi wa Serikali kuweka ukomo huo ili kupunguza matumizi yasiyo na tija. Pinda, amelieleza Bunge kuwa, Serikali inaendelea kupunguza matumizi hayo hasa ununuzi wa magari makubwa na ya kifahari ambayo gharama za ununuzi na uendeshaji ni kubwa sana. Waziri Mkuu amewaeleza wabunge kuwa, kuanzia sasa magari yatakayonunuliwa ni yale yasiyozidi ukubwa wa injini wa CC 3,000 kwa viongozi na watendaji wakuu na yasiyozidi CC 2,000 kwa watumishi wengine wanaostahili kutumia magari ya serikali. Kwa mujibu wa Pinda, ili kupunguza matumizi ya magari kwa viongozi na watendaji wakuu kwa safari za mikoani, Serikali itaanzisha vituo vya kanda vya magari ya serikali yatakayotumika mikoani kwa shughuli za kikazi. “Mwongozo wa utekelezaji utatolewa. Inategemewa kuwa utaratibu huu utapunguza matumizi ya fedha za Serikali kwa kiwango kikubwa” amesema Pinda bungeni mjini Dodoma wakati anasoma mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (Chadema), amesema, kuna watanzania wanaishi kama wafalme na kuna matumizi yasiyo ya kawaida serikalini. Wenje amehoji, wakuu wa mikoa yote nchini wamekwenda Dodoma kufanya nini? Zimetumika fedha nyingi kuwasafirisha, wanalipwa fedha za safari na wanakaa bungeni ‘kula kiyoyozi’ bila sababu za msingi. Kwa mujibu wa Wenje, wakuu wa mikoa wapo Dodoma tangu Jumamosi iliyopita, na wameacha kazi walipotoka. “Wakuu wa mikoa wamekuja kufanya nini? Wamekuja kutafuta nini, wamekuja kutafuta nini?” amehoji Wenje na kusema, Serikali inapaswa kubadili mbinu za kiutendaji.

Mbunge ataja majina ya 'wezi' bungeni

MBUNGE wa Viti Maalum, Riziki Lulida (CCM) leo ametaja bungeni majina ya watendaji wa Halmashauri nchini wanaodaiwa kuiba mamilioni ya fedha za Serikali. Mbunge huyo amepinga kitendo cha mmoja wa watendaji hao kuhamishiwa mkoani Lindi na amesema, mkoa huo si kichaka cha wezi. Ametaja jina la Joachim Materu, na kudai kuwa, mtumishi huyo wa umma aliiba shilingi milioni 557 za umma na amehamishiwa mkoani Lindi. Amewaeleza wabunge kuwa, kitendo cha kuwahamisha wanaodaiwa kuwa ni wezi kutoka Halmashauri moja kwenda halmashauri nyingine ni njama za kudhoofisha maendeleo ya maeneo wanapopelekwa. Lulida amekataa kuunga mkono bejeti ya Waziri Mkuu hadi Materu ahamishwe Lindi. Mbunge huyo amesema kuwa, kuna maofisa mipango Ofisi ya Waziri Mkuu wanaouhujumu Mkoa wa Lindi. Lulida amedai kuwa maofisa hao ni wachaga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), akaomba Kiti cha Spika kimuamuru afute kauli yake ya kutaja kabila la wahusika kwa kuwa Kanuni za Bunge haziruhusu, amefuta. “Suala la uchaga halimo lakini nimetaja majina ili uonekane mtandao”amesema Mbunge huyo wakati anachangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Mbunge huyo amemtaja mtendaji mwingine kwa jina la Yunus Maro, na kudai kuwa, ameiba shilingi milioni 262 za umma, na kutaja akaunti yake ni namba 20660017 iliyopo katika benki ya NMB. Ametaja jina lingine moja la Ndaskoi na kudai kuwa mtumishi huyo ameiba fedha za umma wilayani kilosa mkoani Morogoro na amehamishiwa Ngorongoro. Amemtaja mwingine kwa jina la Macha na kudai kuwa, ameiba mamilioni wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, na ametoa vielelezo kwenye kiti cha Spika wa Bunge kuthibitisha anayoyasema. Lulida amedai kuwa kuna mtandao wa wezi katika Halmashauri nchi wanaoihujumu Serikali. Mbunge wa Mchinga, Said Mtanda (CCM) ameunga mkono kauli ya Lulida kwamba kuna mtandao wa wezi katika Halmashauri nchini. “Huu mtandao ndiyo unaodhoofisha Mkoa wa Lindi” amesema Mtanda wakati anachangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Hata hivyo Mtanda amepinga suala la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuonesha kinawajali sana wananchi wa mikoa ya kusini ukiwemo Mkoa wa Lindi. Amesema, ameisoma Ilani ya Uchaguzi ya Chadema, imeutaja mkoa huo mara moja tu, lakini katika Ilani ya CCM mkoa huo umetajwa mara nane. “Hatutaki ndoa za usiku, asubuhi talaka” amesema Mtanda na kuhoji, Chadema walikuwa wapi miaka iliyopita? “Mheshimiwa unapolia hushiki kichwa cha mwenzio, sisi Lindi matatizo yetu tutayamaliza sisi kwa kushirikiana na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi” amesema Mtanda. .... Source Habari leo

Muslim woman barred from school parents' event for wearing veil

A British Muslim woman was asked to leave a school's parents' night in Manchester for wearing the veil. The college cited "safety" and "security" reasons. Maroon Rafique was stopped from entering Manchester College by security staff, who told her that for the security of teachers and pupils, there was a ban on any kind of face covering. Although she offered to sit anywhere in the room where as few people as possible would see her, she was not allowed onto the campus. “I’m born in this country and British. Why should what I wear offend anyone?” she told the British newspaper the Daily Mail. “I didn’t want to make any fuss. All I wanted was to find out the information to help my son go to university.” The 40 year-old has worn the face veil, or niqab, for the last seven years. Rafique eventually had to phone her husband to take her place. A college spokesman defended the policy. “At all times we need to be able to identify all individuals easily in order to maintain safety and security and therefore we ask that faces are clearly visible while indoors. Our dress code is reviewed through our quality improvement group and we will take this situation into account at the next review.” He added that the school took Rafique's concerns “very seriously.” A spokesman for the Muslim Council of Britain told RT that it considers the decision to be authoritarian. “Wearing the face veil is not obligatory, and is a freedom of choice issue. We understand if teachers are forbidden from wearing it as it can sometimes interfere with communication during the lesson. Children may also have to follow a particular dress code, but for a parent to be stopped doesn’t make sense.” In March of this year, a Muslim woman was stopped from sitting on a UK jury in a murder trial because the judge ruled her facial expressions could not be seen. Britain, unlike France, has not yet introduced a nationwide ban on face veils. ... source RT

'Islamic Awakening': Morsi’sEgypt turns to Iran - report

Newly-elected Egyptian President Mohammed Morsi will rekindle dormant ties between Egypt and Iran and re-consider his country’s peace accord with Israel, according to a controversial interview with an Iranian news agency. Tehran’s Fars news agency distributed a set of quotes from an interview taken hours before Morsi was proclaimed victor in the presidential poll after a prolonged vote count. The views expressed by Morsi contradict his official stance that he will adhere to Egypt’s international obligations. Instead, he reportedly promises to radically adjust the country’s international role. A day after the interview was published, Morsi’s spokesman denied that it ever took place. “We must restore normal relations with Iran based on shared interests, and expand areas of political coordination and economic cooperation because this will create a balance of pressure in the region,” Morsi allegedly told Fars. The two countries broke their diplomatic ties in 1980, following the Islamic Revolution in Iran, and Egypt’s recognition of Israel. Whether or not the interview took place, Iran has welcomed the outcome of Egypt's election. The country’s Foreign Ministry called Morsi’s victory over his secularist rival Ahmed Shafik “an Islamic Awakening” and said the country was entering a “new era.” “The historic Egyptian nation, with their responsible participation in the momentous election, have again proved their determination to realize the noble and justice-seeking ideals of the great revolution of Egypt with a splendid vision of democracy,” read an official statement. Shiite Iran and Sunni Egypt are not historic allies, but Iran’s spiritual leaders and Egypt’s Muslim Brotherhood, to which Morsi belongs, are united by their belief that Islam should play a key role in governance, not to mention a common adversary – Israel. Israel alarmed Several news agencies also reported that Mohammed Morsi intends to review the Camp David accords. Camp David was the site for key meetings between Israeli and Egyptian leaders that climaxed in Egypt becoming the first Arab state to recognize Israel’s right to exist in 1979. The Israeli media struck a uniformly funereal tone in response to Egypt’s choice of leader. “From our standpoint, when the presidential palace in Cairo is painted for the first time in Islamic colors, this is a black and dark day,” wrote commentator Smadar Peri in the popular daily Yediot Aharonot. “Israel should be prepared for every eventuality,” wrote analyst Alex Fishman, conjuring the possibility of “an Islamist intelligence minister, a re- examination of the peace accords, a collapse of the economic agreements and lack of security coordination.” Several other commentators in Israel and in Europe sounded more sanguine, however, noting that while Morsi may wish to change his country’s foreign policy vector, he will have to establish legitimacy in his divided and economically-troubled country before asserting himself internationally. "What he wants tio do is one thing, what he is able to do is another" Professor Daoud Khairallah of Georgetown University told YOU And I blogspot

Monday, June 25, 2012

Former US president Jimmy Carter has criticized America’s actions against terrorism, saying that drones attacks and targeted assassination of suspicious people are undermining America’s “role as the global champion of human rights.” In his critical article "A Cruel and Unusual Record" published in the New York Times, Jimmy Carter said that with all the revolutions sweeping around the world, America should “make the world safer.” Instead, however, “America’s violation of international human rights abets our enemies and alienates our friends,” he argues. US’s government counterterrorism policies, Carter says, are now clearly violating at least 10 of the 30 articles written in the Universal Declaration of Human Rights. “Revelations that top officials are targeting people to be assassinated abroad, including American citizens, are only the most recent, disturbing proof of how far our nation’s violation of human rights has extended,” Carter writes. These violations of human rights began after the terrorist attack of 9/11. Having been "sanctioned and escalated by bipartisan executive and legislative actions,” Carter bemoaned a “lack of dissent from the general public". "As a result, our country can no longer speak with moral authority on these critical issues," the 39th president wrote. Carter says that “death of innocent women and children” within drone attacks on those who are said to be “enemy terrorists” are accepted “as inevitable”. However, that is something that “would have been unthinkable in previous times”. “After more than 30 airstrikes on civilian homes in Afghanistan this year, President Hamid Karzai has demanded that such attacks end, but the practice continues in areas of Pakistan, Somalia and Yemen that are not in any war zone,” writes Carter. He adds that it is unknown “how many hundreds of innocent civilians have been killed” in attacks that have all been “approved by the highest authorities in Washington.” “Top intelligence and military officials, as well as rights defenders in targeted areas, affirm that the great escalation in drone attacks has turned aggrieved families toward terrorist organizations, aroused civilian populations against us and permitted repressive governments to cite such actions to justify their own despotic behavior,” writes Carter. Carter’s critical article comes less than a week after the UN’s report on the use of drone strikes by the US to combat terrorism. On June, 21, UN rapporteur, Christof Heyns, said that the US needs to be held legally accountable for the use of armed drones. He requested that the Obama administration publish statistics on the number of civilian deaths caused by strikes on suspected terror leaders in Afghanistan, Pakistan and Yemen. Heyns underlined the fact that recent US drone strikes threatened the rule of international law in that many “targeted killings take place far from areas where it's recognized as being an armed conflict." Speaking about human rights, Carter also mentioned that recent laws allow “unprecedented violations of our rights to privacy through warrantless wiretapping and government mining of our electronic communications”. Jimmy Carter has called for Washington to “reverse course and regain moral leadership".

we will be back very soon

blog yenu ya ukweli ipo karibuni kurudi tena hewani..... Ushirikiano wenu ni muhimu sana kwetu