Sunday, March 8, 2015

''JIHAD JOHN'' Chinja chinja wa IS alifukuzwa Tanzania


Mohammed Emwazi ,mtu ambaye alibadilika na kuwa ''chinja chinja'' wa kundi la islamic state kwa jina 'jihad John' Mohammed Emwazi, alifurushwa kutoka nchini Tanzania kwa kuwa mlevi na mtu anayetoa matusi.,afisa moja wa polisi ameiambia BBC. Emwazi anasema alitishiwa na kuhojiwa chini ya maagizo ya shirika la upelelezi la Uingereza MI5 alipoenda nchini humo mwaka 2009 Lakini BBC imeonyeshwa rekodi za kuzuiliwa kwake tangu alipokamatwa. Afisa huyo amesema kuwa Emwazi hakuruhusiwa kuingia nchini Tanzania kwa sababu alikuwa amezua mgogoro katika uwanja wa ndege na kuwa na tabia za mlevi. Emwazi ambaye ana zaidi ya miaka 20 na ambaye anatoka magharibi mwa London ametambuliwa kama mtu aliyeziba uso katika kanda kadhaa za video ambapo mateka wamechinjwa. Emwazi amesema kuwa alikuwa mwanafunzi ambaye alikuwa katika likizo ya safari wakati aliposafiri na kuingia Afrika mashariki kupitia uwanja wa ndege wa Dar-e-salaam kutoka nchini Uholanzi miaka sita iliopita.

No comments:

Post a Comment