Sunday, March 1, 2015

Uchaguzi wa bunge waahirishwa Misri

Tume ya uchaguzi ya Misri inasema kuwa inatayarisha ratiba mpya ya uchaguzi wa wabunge ambao ukitarajiwa kufanywa badaae mwezi huu. Hapo awali mahakama kuu ya Misri yaliamua kuwa sehemu ya sheria kuhusu uchaguzi inakwenda kinyume na katiba na hivo kuzusha uwezekano wa kucheleweshwa. Rais Abdul Fattah al-Sisi alijibu hukumu hiyo kwa kuamrisha kuwa sheria mpya kuhusu uchaguzi itayarishwe katika mwezi mmoja. Bunge la Misri lilivunjwa mwaka wa 2012 baada ya kufutwa na mahakama. Na wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri imewasamehe na kuwaachilia huru wafungwa 68 kufuatana na msamaha aliotoa rais. Rais Abdul Fattah al-Sisi alitoa amri hiyo mwezi wa Januari kuadhimisha miaka mine baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani Rais Hosni Mubarak. Wafungwa wengine 72 wamefunguliwa kwa shuruti wasivunje sheria tena. Inafikiriwa kuwa wengi walioachiliwa huru walikuwa wafungwa wa kisiasa. Tangu Rais Sisi kushika madaraka waandamanaji kama 1,400 wameuliwa na askari wa usalama, na kama 40,000 wamekamatwa - wengi wao wanashutumiwa kuwa Waislamu

No comments:

Post a Comment