Monday, March 2, 2015

Vikosi vya kuzima moto vyapata wakati mgumu kuzima moto Cape town

Zaidi ya helikopta 8 na magari 40 ya zimamoto na askari wa kikosi cha kuzima moto wapatao 200 wako katika jitihada za kuuzima Moto mkubwa unaowaka katika maeneo ya milima ya Muizinberg mjini Cape town,Moto huo ambao ulianza usiku wa jumapili umekuwa ukiwashinda nguvu kikosi hicho kutokana na upepo mkali unaovuma eneo hilo.! Mashuhuda wanasema kuwa watu wote wanaoishi maeneo yanayozunguka Eneo la moto wamehamishwa na kupelekwa eneo salama.! Mpaka sasa bado hakuna matumaini ya kuuzima moto huo ambapo helikopta za kuzima moto zimeonekana zikinyonya Maji katika Mabwawa ya kuogelea(swimming pools) katika maeneo hayo ili kurahisisha uzimaji wa moto huo..!

No comments:

Post a Comment