Wednesday, August 3, 2011

MUSEVEN AITISHA KIKAO KUNUSURU UCHUMI WA UGANDA

Rais Yoweri Museveni ameitisha
kikao cha dharura cha mawaziri
kujadili jinsi ya kukabili nhali
mbaya ya uchumi nchini humo.
Baraza hilo la mawaziri
linakutana katika kipindi
ambacho viongozi wa upinzani
wamekuwa wakilalamikia
kupanda kwa gharama za
maisha.
Bidhaa muhimu kama vile sukari
zimeanza kukosekana madukani
hali ambayo inawaathiri watu
wenye kipato cha chini nchini
humo.
Bei ya sukari imepanda
kiasi kwamba kile kiasi kilichoko
aidha kinafichwa ama
kuniauzwa bei kali ambayo sio ile
ya kawaida.
katika maduka makubwa watu
hawakubaliwi kununua zaidi ya
kilo moja.
Hali hii inatishia uchumi wa taifa
ambao kwa sasa kwa mujibu wa
gavana wa benki kuu ya taifa
kiwango cha ukuaji wa uchumi
wa Uganda kitadidimia kwa asili
mia 5 kutokana na kiwango
kikubwa cha mfumuko wa bei za
bidhaa.
Mfumuko wa bei unakaribia asili
ia 20, kiwango kikubwa zaidi
kwa kipindi cha maiaka 10.
Pia kiwango cha ubadilishanaji
wa pesa za Uganda kwa dola
kumepanda kiasi kuwa dola 1
inanunua shilling za Uganda
2,634.
Msemaji wa serikali na waziri wa
habari bi Mary okurut amesema
kikao hicho maalum cha
mawaziri kitajadili mikakati ya
kukabili hali hii ya uchumi.
Kuhusu kutoweka kwa sukari
madukani, waziri Okurut
amesema kuwa serikali imeomba
ruhusa kutoka jumuiya ya Afrika
mashariki ikubaliwe kuagizia
sukari kutoka nje ya ukanda huu.
Uganda ina viwanda vitatu
vinavyozalisha sukari, lakini ni
kimoja tu kwa sasa kinachofanya
kazi.
Viwili vilivyosalia, kimoja
kimefungwa kwa sababu
mitambo yake inafanyiwa
ukarabati ilhali kingine kwa
kuwa hakipati miwa
inayotosheleza uzalishaji.

No comments:

Post a Comment