Monday, June 13, 2011

KATIBA YA ZANZIBAR KUWASILISHWA LEO

WAZIRI wa Fedha wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Omar Yussuf
Mzee leo Jumatano
atawasilisha bajeti ya serikali
kwa mwaka 2011/12 huku
wafanyakazi wa serikali wakiwa
na matarajio ya kuongezewa
mishahara yao.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi
Ibrahim Mzee alisema juzi kuwa
bajeti hiyo itasomwa kuanzia saa
10 jioni katika kikao hicho cha
bunge ambacho kitaketi kwa
wiki sita.
“Hatujajua kilichomo kwenye
hotuba ya bajeti, lakini katika
mkutano huo wa Bunge maswali
237 yataulizwa na wawakilishi
na kujibiwa na mawaziri,”
alisema katibu huyo.
Hiyo itakuwa ni bajeti ya kwanza
tangu kuundwa kwa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa (GNU)
inayohusisha mawaziri kutoka
vyama vya CCM na CUF. Waziri
Mzee juzi jioni alitarajiwa pia
kuzungumza na waandishi wa
habari juu ya mweleko wa bajeti
hiyo.
Baadhi ya wachambuzi wa
mambo wametaka bajeti hiyo
ijielekeze zaidi kumpunguzia
mwananchi wa kawaida makali
ya maisha, ikiwa ni pamoja na
kupunguza mfumuko wa bei na
pia ijielekeze katika kuboresha
masuala ya kilimo, afya na elimu.
Ili kukifanya kikao hicho
kisikwame kutokana na matatizo
ya umeme, katibu huyo alisema
tayari ofisi yake imeshanunua
jenereta la dharura lenye uwezo
wa kutoa kilovoti 7.25 za umeme
ambalo limenunuliwa kwa
thamani ya Sh milioni 355.
Alisema jenereta hilo litawasili
kisiwani hapa wakati wowote,
“Na pia tumetumia Sh milioni sita
kwa ajili ya kupunguza
mwangwi kwenye ukumbi wa
baraza.”
Tangu kufunguliwa kwa ukumbi
mpya wa baraza la wawakilishi,
wajumbe wa baraza la
wawakilishi wamekuwa
wanalalamika kwa spika kuwa
mawasiliano ndani ya ukumbi
huo ni magumu kutokana na
kuwepo kwa mwangwi pamoja
na kutokuwepo na jenereta la
dharura.

No comments:

Post a Comment