Tuesday, June 14, 2011

MKULO;SINA UWEZO WA KUONDOA POSHO

Wakati wanaharakati wakipinga,
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo,
amesema hana uwezo wa
kuondoa posho za Mbunge wa
Kigoma Kaskazini (Chadema),
Zitto Kabwe, na wenzake wa
NCCR- Mageuzi wanaotaka
ziondolewe.
Akizungumza mjini
Dodoma jana, Mkulo alisema
Baraza la Mawaziri pekee ndilo
lenye uwezo wa kutengua sheria
hiyo na si yeye hivyo
wanaomtaka azihamishe
hawajui wanachosema.
" Mimi Mkulo sina uwezo wa
kubadilisha maamuzi ya baraza la
mawaziri hata siku moja, suala
likishaamriwa kule mtu binafsi
huna uwezo wa kulitengua,
labda niende kwenye baraza hilo
nijenge hoja wakubali,” alisema.
Katika hatua nyingine, Mkulo
alishangaa hatua ya wabunge
wanaokataa posho hizo
zipelekwe kwenye majimbo yao
badala ya kuiachia serikali
uamuzi.
" Kama wanataka zifutwe
waseme, lakini kusema ziende
sehemu fulani haina maana,
kama kweli wanataka kubana
matumizi waseme posho hizi
zifutwe na wafuate taratibu
maana ziko kwa mujibu wa
sheria za nchi,”alisisitiza Mkulo.
" Zitto ni mjumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge kama kweli
hataki hizi posho angesema kule
zikatwe sasa mbona alishiriki
kuzipitisha? "alihoji.
Wabunge wa Chadema na
wengine wanne wa NCCR-
Mageuzi wote kutoka majimbo
ya Mkoa wa Kigoma, wanataka
posho hizo zifutwe.
Akizungumzia posho hizo za
vikao, Mbunge wa Vunjo (TLP),
Agustine Mrema, alisema kwa
kuwa serikali ilishatangaza katika
bajeti yake kuwa itapunguza
posho zisizo za lazima, basi
itaangalia kama posho za
wabunge nazo hazina ulazima.
" Mimi naunga mkono posho
zisizo za lazima ziondolewe,
kama serikali itaona posho za
wabunge si za lazima na
ikaziondoa mimi sina neno,
wakiona mbunge anaweza kuja
hapa Dodoma na akafanya kazi
zake bila kuhitaji hiyo posho
sawa mimi nasubiri uamuzi wa
serikali,” alisema.
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad
Rashid, alisema kuwa: " Katiba
inatamka wazi kwamba mtu
akifanya shughuli hii malipo yake
ni haya sasa tatizo ni nini."
Alisema kama wanaopokea
posho hizo wanaona hawana
haja nazo waandike hundi na
kuzirejesha zilikotoka badala ya
kupiga kelele kwenye vyombo
vya habari.
" Hizo ni cheap politics (siasa
uchara) ambazo mimi binafsi
sizitaki na kamwe sitazishabikia,
mbona wanapokwenda kwenye
halmashauri kule wanasaini
posho iweje wakija huku ndipo
waseme hawazitaki, maoni
yangu ni kwamba tukiamua
kubadili sheria na kuziondoa
sawa sitakuwa na tatizo, lakini
kwa kuwa sasa hivi ziko kisheria
tatizo linatokea wapi,” alisema
Rashid.
Spika wa Bunge, Anne Makinda,
alisema kuna watu wanapotosha
kuwa mshahara wa mbunge ni
zaidi ya milioni saba wakati
mshahara halisi ni Sh. milioni 2.5
na wanakatwa Sh. 900,000 kila
mwezi kwa ajili ya mikopo ya
magari waliyochukua.
KWA HABARI ZAIDI SOMA GAZETI LA NIPASHE LA LEO TAREH 13 JUNE

No comments:

Post a Comment