Thursday, June 23, 2011

MKULIMA ATUHUMIWA KUMBAKA MWANAFUNZI

POLISI mkoani Singida
wamemkamata mkulima, Iddi
Ramadhan (20) mkazi wa kijiji
cha Matyuku Singida Vijijini, kwa
tuhuma za kumbaka mwanafunzi
wa shule ya sekondari na
kumsababishia maumivu makali.
Kamanda wa Polisi mkoani
humo, Celina Kaluba, amesema,
Ramadhan alikamatwa Juni 18
mwaka huu saa moja jioni katika
kitongoji cha Makyunje, Kata ya
Mtamaa tarafa ya Unyakumi
Manispaa ya Singida.
Amesema, mtuhumiwa anadaiwa
kumkamata kwa nguvu binti
huyo mwenye miaka 15, kumziba
mdomo na kumkokota hadi
kichakani na akamvua nguo yake
ya ndani na kumfanyia unyama
huo.
Kamanda Kaluba amesema, mara
baada ya kukamilika kwa
upelelezi, mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma inayomkabili.
Katika tukio lingine, Kaluba
amesema, Polisi wamemkamata
mkulima mkazi wa Mang'onyi,
Singida Vijijini, Saidi Msengi (22)
kwa tuhuma ya kumgonga kwa
pikipiki mwendesha baiskeli,
Polino Michael na kusababisha
kifo chake.
Alieleza kuwa siku ya tukio,
mtuhumiwa alikuwa akiendesha
pikipiki aina ya Sanlag T.708 BRP
na alimgonga mwendesha
baiskeli huyo Michael (50)
mkulima na mkazi wa kijiji cha
Matare.
Alisema, Polino alifariki dunia
akiwa njiani kwenda hospitali ya
mkoa kupatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment