Sunday, August 12, 2012

MISRI YATUMA VIKOSI VYAKE SINAI

Misri imetumia Helicopter kufanya mashambulizi ya mizinga dhidi ya wakereketwa wenye imani kali walio katika eneo la Sinai tangu mwaka 1973 katika kile jeshi la Misri lililochotaja kama shambulio la kurejesha utulivu. Matumizi ya anga ni ishara ya mabadiliko ya vita vya Misri dhidi ya wakereketwa wa Kiislam ambao wamezidisha shughuli zao katika eneo lenye milima na jangwa lenye mpaka na Israili na Gaza. Mapema wiki hii wapiganaji wakereketwa waliishangaza Misri kwa ujasiri wao kwa shambulizi ambamo askari 16 waliuawa, magari ya jeshi yakaibwa na kuelekea Israel kwa lengo la kujaribu kufanya shambulio jingine. Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa jeshi limesema kua limeanzisha operesheni ya mchanganyiko wa vikosi kwa kutaka kurejesha utulivu huko Sinai, majeshi yakiungwa mkono na Jeshi la anga. Shambulio la siku ya jumapili ndio baya kuwahi kufanywa huko Sinai kwa miaka mingi na hatari kuliko yote dhidi ya vikosi vya Misri ikiashiria ongezeko la vitendo vinavyokiukaq sheria katika eneo hilo. Katika tukio la hivi karibuni, watu wenye silaha waliwafyatulia risasi walinzi kwenye vizuizi huko El -arish, mji mkuu wa Wilaya ya Sinai, mji ulio umballi wa kilomota 50 kutoka mpaka wa Gaza na Israili. Ghasia kwenye mpaka wa Israel na Misri inaweza kutishia mkataba wa amani baina ya nchi hizi mbili. Hio ndio sababu Israel imeiambia Misri ichukue hatua za kusuluhisha vurugu badala yake kupeleka vikosi vyake. Israel imekubali kuondoa baadhi ya masharti yanayozuwia shughuli za kijeshi katika Sinai ili Wa Misri waweze kuingiza vikosi zaidi. Lakini uvamizi wa Misri dhidi ya kile walichokiita magaidi hautobadili lolote katika sehemu ya Sinai inayokaliwa na makabilia ya Wa Bedwini wenye fikra huria. Ni eneo linalovutia kwa makundi ambayo yangependa kutumia sehemu isiyokua na utaratibu wowote wa uongozi kwa aijili ya kuifika Israili.Rais wa Misri Mohammad Mursi aliahidi kwamba atadhibiti eneo la Sinai kwa ukamilifu.

No comments:

Post a Comment