Sunday, August 12, 2012

Wakenya 13 wafariki dunia katika ajali ya mabasi ilotokea tanzania

Idadi ya watu walofariki katika ajali ya mabasi mawili karibu na mji wa Tanga Tanzania Ijuma asubuhi imefikia 13. Watu 42 wamejeruhiwa miongoni mwao 14 wako katika hali tabani, watu 29 hawakujeruhiwa. Walofariki ni miongoni mwa kundi la wanawake wa Kenya kutoka kanisa la Presbyterian Church of East Africa - PCEA kutoka Thika walokuwa wanasafiri kuelekea Dar es Salaam kwa sherehe za kidini Tanzania. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani Tanzania, Ernest Mangu ameiambia sauti ya Amerika kwamba serikali ya Kenya inashirikiana kwa karibu sana na Tanzania na imepeleka ndege maalum kuwasafirisha nyumbani walonusurika.

No comments:

Post a Comment