Monday, August 13, 2012

Uraiqat ataka Palestinaitambuliwe rasmi UN

Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono uwanachama wa Palestina kama nchi huru katika Umoja wa Mataifa. Saeb Uraiqat kiongozi wa timu ya mazungumzo ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina leo ameitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono ombi litakalowasilishwa tena na PLO, la kutaka Palestina iwe nchi mwanachama inayojitegemea katika Umoja wa Mataifa. Huku akiashiria kwamba nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu zinaunga mkono kutambuliwa rasmi Palestina kama nchi huru, Uraiqat amesisitiza kuwa, Mamlaka ya Ndani ya Palestina itaendelea na jitihada zake za kufanikisha suala hilo licha ya mashinikizo mengi yanayoikabili. Mwaka uliopita Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alitoa pendelezo la kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina kwa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa lakini kutokana na uungaji mkono wa Marekani kwa Israel na ushawishi wa tawala hizo kwenye umoja huo, pendekezo hilo halikupitishwa.

No comments:

Post a Comment