Monday, August 13, 2012

Tanzania Vs Malawi

MGOGORO wa siku nyingi wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Serikali ya Tanzania na Malawi umeibuka kwa kasi baada ya kuwa umetulia kwa muda mrefu. Akiwa Bungeni hivi karibuni kuwasilisha hotuba ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bw. Bernard Membe, aliionya nchi ya Malawi kusitisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi katika ziwa hilo. "Serikali iko tayari kulinda mipaka kwa gharama yoyote ile na inaitahadharisha Serikali ya Malawi kuondoka mara moja na kusitisha shughuli zozote zile za utafiti ndani ya Ziwa Nyasa ndani ya nyuzi 11 hadi 9, kwani sehemu hiyo ni mali ya Tanzania," alisema Bw. Membe. Bw.Membe aliongeza kuwa Tanzania itakuwa tayari kutumia gharama zozote kulinda mipaka yake na kuitaka Malawi kuacha mara moja kuendelea kutoa vibali kwa kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta na gesi. Eneo hilo la mwambao wa Ziwa Nyasa, Bw. Membe alisema, linatumiwa na wakazi zaidi 600,000, ambao maisha yao ya kila siku yanategemea ziwa hilo, hivyo kamwe Serikali haitakubali kuona wananchi wake wakinyanyasika. Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Frederick Werema alinukuliwa na 'Daily Times' la Malawi akimjibu Mbunge wa Mbeya (Vitu Maalum), Bi. Hilda Ngoye, akisema, ÒHatutaki Watanzania waombe ruhusa kutoka Malawi kuchota maji au kuvua Ziwa Nyasa. Kama hatufikii makubaliano tunalipeleka suala hili kwenye sheria za kimataifa.Ó Bi. Ngoye alidai kwamba watalii wa Malawi na boti za uvuvi zimekuwa zikiingia kwenye eneo la maji ya Tanzania kadri wanavyotaka. âÓWatanzania wanaoishi kuzunguka Ziwa Nyasa wanahaki ya kuvua na kufanya shughuli nyingine za uzalishaji katika ziwa hilo, bila kupewa vitisho,Ó Bi. Ngowe aliliambia Bunge la Tanzania, akitaka maelezo kutoka Serikalini kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi. Kwa upande wake, mwandishi Bw. Cedrick Ngalande wa gazeti la 'Malawi Times' la Agosti 6,2012 aliandika katika maoni yake akidai kwamba wakati wa Uhuru watu wachache nchini Tanzania walitaka kumega sehemu kubwa ya Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) kama wanavyoliita wenyewe. Alisema wakati wa enzi za utawala wa Dkt Kamuzu Banda, Tanzania haikuwahi kuzungumzia wazo la kuligawa ziwa na suala hilo lilikuwa karibu limesahaulika kabisa wakati wa utawala wa Dkt. Bakili Muluzi na hata baadaye. Aliendelea kuhabarisha kwamba marehemu Dkt. Bingu wa Mutharika aliipa jukumu kampuni moja kuanza kazi ya utafutaji mafuta katika ziwa hilo na Tanzania haukusema lolote wakati huo na ndicho chanzo cha kuibuka mgogoro huo. "Sasa tuna Rais mpya na ghafla Watanzania wanataka kwamba Serikali iache kufanya shughuli zote za utafutaji mafuta katika ziwa hili mpaka masuala yote yanayohusiana na mipaka yametolewa ufafanuzi. Kwa nini iwe sasa? Alihoji Bw. Ngalande. Bw. Ngalande alisema wakati Bi. Joyce Banda alipotwaa madaraka ya urais, ilionekana kwamba Malawi sasa itatekeleza kila kitu anachoagizwa kufanya Bi. Banda na Jumuiya ya Nchi Hisani. Mwandishi huyo alisema baadhi ya magazeti ya Uingereza yalishangazwa sana na hali hiyo kiasi cha kuwaita watu wa Malawi ÓTaifa linaloogopa wafadhiliÓ. Alisema Rais Joyce Banda aliwahi kwenda London na hata kumpigia magoti Malkia Elizabeth, ambayo ni ishara ya ajabu sana na ukitilia maanani wote wawili ni wakuu wa nchi. "Sawa, maneno yote haya na matendo ukiyajumuisha pamoja yanatoa picha ya uongozi dhaifu wa Malawi. Dunia imenusa harufu ya damu. Sasa Tanzania imeamua ni wakati wa kuligawa ziwa. Kumbuka kwamba hawakulileta wazo hili wakati Bw. Muluzi au Bw. Mutharika walipokuwa madarakani," alisema Bw. Ngalande. "Kama tutaipa Tanzania heshima kusikiliza ombi lake, mtu atashangaa ni kitu gani kitakachofuata baadaye. Je, sasa watadai Chitipa (wilaya ya kaskazini mwa Malawi)? Je, Msumbiji nayo itadai Mlima Mulanje ni wa kwake? Bw. Ngalande aliendelea kuhoji. "Serikali ni lazima iweke wazi kwamba hakuna sehemu yoyote ya Malawi ifanyiwe mjadala Òkwisha!Ó Sasa ni wakati wa kuonesha uwezo wetu. Iambie Tanzania kwamba Ziwa Malawi siku zote lilikuwa, limekuwa na litakuwa la Malawi," aliandika katika maoni yake. "Cha kushangaza, baada ya maelezo yote haya ya kiburi cha Serikali ya Tanzania, jibu la Serikali yetu (Malawi) limekuwa hafifu. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje (Malawi) ametoa kauli akisema suala hilo litatatuliwa ÓkirafikiÓ. "Kweli, Mhe. Waziri? Nini maana ya maelezo ya kirafiki? Je, unapanga kuligawa ziwa na kuipa heshima Tanzania kwa matakwa yasiyokuwa na msingi? Utawezaje kuwa na utatuzi wa amani kwa madai yasiyokuwa ya msingi? Alihoji zaidi Bw. Ngalande. Kwa upande wake, Bw. Patrick Kabambe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Malawi alinukuliwa na gazeti la 'Daily Times' la Malawi. Bw. Kabambe alitoa kauli ya ajabu akisema, ÒMadai yetu yako wazi juu ya suala hili. Kwa mujibu wa makubalinano ya ecoland 1890 kati ya Serikali ya Uingereza na Ujerumani, mpaka baina ya Malawi na Tanzania ni kuanzia mwanzo wa maji ya Ziwa Malawi upande wa Tanzania. Kwa hiyo, tunalifahamu fika na tutaendelea kuihusisha Tanzania kama majirani zetu wema.Ó Mgogoro ni kuhusu nani anastahili hasa kumiliki Ziwa Malawi kama linavyojulikana na Wamalawi wengi na Lake Nyasa kama linavyojulikana na Watanzania wengi. Kwa mujibu wa Malawi, hili sio suala la kufanyiwa mjadala. Malawi wakidai wanamiliki asimia 100 ya Ziwa Malawi na kama wataenda kwa mtazamo wa baba yao wa taifa, Dkt. Hastings Kamuzu Banda, Malawi kama ilivyokuwa ikijulikana, Maravi Kingdom, inaweza kutanuka mpaka baadhi ya maeneo ya Tanzania na hata Msumbiji. Kwa mujibu wa Tanzania kwa upande mwingine, ziwa hilo linatumiwa kwa pamoja na mpaka wa nchi hizi mbili unapaswa kufuata mstari wa 'median' katika Ziwa Nyasa. Huu ndio umekuwa msimamo wa Serikali ya Tanzania na shughuli yoyote itakayofanywa na Malawi kupita mstari huu itachukuliwa kama Òkuingia eneo lisilo lakeÓ. Kihistoria mgogoro huu unaanzia Mkutano wa Berlin na tatizo lipo kwenye Sheria ya Bunge la Berlin ya 1885, iliyosainiwa na mataifa 13 yenye nguvu ya Ulaya yaliyohudhuria mkutano huo wa Kuigawa Afrika. Kinyang'anyiro cha kuigawa Afrika Kwa mujibu wa hati za kugawa mpaka kuzunguka Ziwa Nyasa na kusimamiwa na mkataba wa nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Ujerumani tarehe 1, Julai, 1890, Dkt Banda mwaka 1962 aliwahi kudai kwamba sehemu moja ya Msumbiji ilipaswa kuwa ya Malawi, wakati huo ikiitwa Nyasaland. Tanzania nayo inaweza kuonesha ramani zinazoonesha mstari wa 'median' kama mpaka na ramani hizo hazijawahi kwenda kinyume na yaliyomo katika mkataba huo. Mgogoro wa Ziwa Nyasa utakuwa vigumu kufutika siku yoyote hivi karibuni kwa pande zote mbili za Tanzania na Malawi na kabla hata ya Uhuru. Mtu anaweza kushangaa kama Watanzania ni wendawazimu kudai nusu ya ukubwa wa ziwa ambapo waliotengeneza ramani hizo wanaonesha mstari wa 'median' kama mpaka. Kuna baadhi ya mikataba ya kimataifa inayoshughulika na haki zinazohusiana na maji. Kutokana na maelezo ya Bw. Patrick Kabambe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Malawi, ufumbuzi wa suala hili bado ni mgumu. ÒBila shaka, tulifanya majadiliano ya mpaka na tukawaambia Watanzania kwamba kwa jinsi tunavyoelewa, ziwa lote ni mali ya MalawiÓ alisema Bw. Kabambe. Ushauri umetolewa kwamba pande zote mbili za mgogoro huo zinapaswa kukutana na kufikia makubaliano kwa amani. Dkt. Hastings Kamuzu Banda aliwahi kusema, Òsisi sote ni ndugu ramani na mipaka tuliwekewa na wakoloni, kwa hiyo, sisi sote (Wamalawi na Watanzania) tuvue samaki na kuogelea pamoja katika ziwa zuri la Nyasa." Tanzania imekuwa na uzoefu mkubwa ukilinganisha na Malawi katika medani za kivita. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeshiriki mapigano mengi kwa mafanikio makubwa ikiwemo oparesheni dhidi ya wakoloni wa Kireno 1960 nchini Msumbiji. Kama hiyo haitoshi, JWTZ iliwahi kupigana dhidi ya majeshi ya Rhodesia na Afrika ya Kusini (1975-1980) na dhidi ya magaidi wa RENAMO wa Msumbiji 1986-1988. JWTZ iliwahi pia kutoa kipigo kitakatifu katika vita ya Kagera 1978 dhidi ya majeshi ya nduli Iddi Amin wa Uganda, ambapo nduli huyo aliweza kuitoroka nchi yake na kuishi uhamishoni mpaka mauti yalipomkuta. JWTZ pia imeshiriki usimamizi wa kulinda amani pamoja na Majeshi ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, eneo la Darfur nchini Sudan na nchi ya Lebanon.

No comments:

Post a Comment