Thursday, September 26, 2013

Sita na vyombo Vya usalama

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuacha kufanya kazi kwa mazoea, bali viimarishe ulinzi ili kukabiliana kuweza matukio ya kigaidi. Sitta alisema hayo jana baada ya kufungua mkutano wa Chama cha Waajiri Tanzania (Ate) na sekta binafsi. Alisema tukio la ugaidi lililotokea Nairobi nchini Kenya ambalo limesababisha vifo vya watu 62 linaweza kutokea mahali popote ikiwemo Tanzania. “ Ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji, vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi hasa kwenye mikusanyiko ya watu,” alisema. Alisema vyombo vya ulinzi vinatakiwa kuwa macho muda wote ili kukabiliana na hatari yoyote inayoweza kutokea.

No comments:

Post a Comment