Saturday, September 21, 2013

Wizara ya Elimu yatoa Tangazo kwa walimu Tarajali

Wanafunzi waliochaguliwa Orodha ya nyongeza kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa kuanzia Jumapili tarehe 22/09/2013 hadi 29/09/2013. Fomu ya maelekezo (joining instruction) zinapatikana kwenye tovuti hii kwa kubofya hapo chini. Wanafunzi wanatakiwa kufika Vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo: 1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania kidato cha NNE; 2. Ada ya muhula wa kwanza sh. 100,000/= au ya mwaka sh. 200,000/=; 3. Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya Chuo husika; na 4. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi. Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo. Usajili wa kujiunga na Vyuo utafungwa tarehe 29/09/2013 saa 12.00 jioni

No comments:

Post a Comment