Wednesday, September 25, 2013

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SKOLASHIPU ZA MSUMBIJI (TAMOSE) NA UTARATIBU HUSIKA 2014

Wanafunzi 51 wa Kitanzania wamechaguliwa kujiunga na masomo mbalimbali nchini Msumbiji katika ngazi ya Shahada ya Kwanza kupitia Mpango wa Kubadilishana Wanafunzi kati ya Serikali ya Tanzania na ya Msumbiji (Tanzania – Mozambique Students Exchange Programme – TAMOSE). Masomo yanatarajiwa kuanza juma la Kwanza la Januari, 2014. Wanafunzi hao ambao orodha yao na masomo watakayosoma vimeambatishwa, wanatakiwa kufika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara ya Elimu ya Juu, Chumba Namba 28 kwa ajili ya maelekezo na maandalizi ya safari. Wanafunzi hao wafike Wizarani kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 14 Oktoba 2013 kuanzia Saa 3.00  asubuhi hadi saa 9:30 mchana katika siku za kazi. Wanafunzi wanashauriwa kufika na nyaraka za kuombea pasi ya kusafiria nje ya nchi – passport (kwa wale ambao hawana). Nyaraka hizo ni pamoja na Cheti cha Kuzaliwa, Picha 5 za passport size zenye rangi ya buluu ya bahari pamoja na gharama za kuombea hati ya kusafiria nje ya nchi Wizara ya Mambo ya Ndani. Kwa wenye passport wanatakiwa kuja nazo.

No comments:

Post a Comment